Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Vyombo vya Habari nchini wametakiwa kuendesha ajenda ya hali ya Mabadiliko ya hali ya Hewa kuanzia ngazi ya chekechea mpaka ngazi ya chuo.
Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi, Hellen Utaru amesema waandishi wa habari nchini ,wanajukumu la kusadia kutoa elimu jinsi gani wadau wanavyoweza kushirikiana kusaidia jamii katika mabadiliko ya hali ya hewa.
Hellen ameyasema hayo alipokuwa akizungumza katika warsha ya umoja wa Maafisa Watendaji Wakuu Tanzania wakiwemo Mashirika Binafsi na Serikali (CEOrt) wakishirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira (Journalists’ Environmental Association of Tanzania – JET).
Ellen amesema kama kutakuwepo kwa mfumo rasmi wa ufundishaji elimu ya mazingira na uhifadhi kwa watoto, kuanzia chekechekea hadi vyuoni kulingana na mazingira yanayowazunguka itakuwa bora zaidi.
Amesema uzoefu unaonesha watu wanaokua wakiwa katika mazingira chanya (positive) wanakuwa na fikra chanya pia.
Amesema watu wa aina hiyo wanapata nafasi ya kufikiria na kuwa wabunifu kuliko ambao wanakuwa katika mazingira mabovu .
‘”Kwani tunaposema mazingira tunatanua wigo kwa maana ya kuwajumuisha viumbe wote wanaotambaa ,wanaoruka wanaoishi kwenye maji wote hao tunawahitaji kwa mfano kama nyuki wanatuletea asali na matunda sasa tunapokosa matunda tunapata utapia mlopia umasikini”amesema.
Amesema mikakati ya warsha ni kuhakikisha ,sekta binafsi inaweza kukaa na waandishi wa habari na kujadili masuala yote ya mazingira na mabadiliko ya tabia nchi kupata uelewa wa pamoja.
“lakini pia kutafuta namna ya kufikisha elimu ya uhifadhi wa mazingira kwa wananchi, kwasababu sekta binafsi wanawajibika kuboresha mazingira lakini je wanawajibika kwa namna gani na jinsi ya kufanya hizo kazi”amedai.
Amesema uharibifu wa mazingira unaweza kuwa na madhara mengi ya kijamii ambayo yanaweza kuathiri watu wengi.
Hellen ameshauri waandishi kubadilika mfumo wa utoaji taarifa, katika vyombo vyao kutoka kwenye wakati wa tatizo linapotokea kwenda kwenye elimishaji jamii juu ya uhifadhi wa mazingira.
“Watu wanachukulia suala zimala utunzaji wa mazingira ni kupanda miti na usafi ,kuna vitu vingi mungu ametupa kwa hiyo tunataka vyombo vya habari kusadia kutoa kwa elimu wananchi juu ya umuhimu wa uhifadhi.
Mkurugenzi mtendaji John Chikomo, amesema taasisi hiyo, imefanikiwa kwa kiasi kikubwa katika suala zima la uhifadhi wa mazingira na elimu kwa waandishi na jamii.
Amesema JET imefanikiwa kuwa kupeleka mbele, agenda ya mazingira na mabadilko ya tabia nchi climate change,kwa kutoa mafunzo wandishi wa habari kutoka bara na visiwani kutoa elimu ya kwa jamii.
“Tumewapatia elimu juu ya kuandika mabadiliko ya tabia nchi, migongano ya binadamu na wanyamapoli kwa jamii uhifadhi wa bionuai.
Mpaka sasa tayari tumefikisha zaidi ya waandishi 400 na kila mwaka, waandishi 25 wanapata nafasi ya kuingia katika mafunzo ya uhifadhi, wapo ambao wanajirudia lakini wengine wapya.
Tumeweza kupambania suala zima la uhifadhi utunzaji wa mazingira kwa mfano bonde la Ihefu, tulianza kazi mwaka 1999.
Kama JET tulihakikisha wafugaji ambao walikuwa wamevamia lile bonde la Usangu ,wanaondoka na mto Rufiji, linatunzwa sasa hivi tunajivunia bwawa la umeme mkubwa la Mwalimu Nyerere.
Ameshauri waandishi wa habari wale waliopata mafunzo kutoka JET, kuhakikisha wanaelimisha umma juu ya suala zima la uhifadhi.
“Kupitia mkuano huu tunategemea waandishi watahabarisha umma hasa wafanyabishara wajue kwamba biashara na mabadiliko ya tabia nchi ni vitu vinavyokwenda sambamba”amesema
Chikomo amesema wafanyabiashara wakubwa na makampuni makubwa, yana nafasi ya kuhakikisha wanapeleka mbele ajenda ya mabadiliko ya tabia nchi katika kazi zao au shughuli zao za kila siku.