Na Magrethy Katengu, JamuhuriMedia, Dar es Salaam

VIONGOZI wa Vyama vya CUF, UDP, NCCR Mageuzi na NLD wamesema wamevutiwa na namna Serikali ya Awamu ya Sita iliyo chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya mfumo wa 4R na mabadiliko makubwa aliyoyafanya ya kidiplomasia nchini l.

Wamesema hivyo wapo tayari kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu, na Uchaguzi Mkuu mwakani na hawana mpango wa kususia .

Falsafa ya 4R ya Rais Samia imejikita kwenye Maridhiano, Diplomasia ,Ustahimilivu, Mabadiliko na Kujenga Upya.

Wakizungumza Oktoba 8, 2014 Dar es Salaam ofisini kwao baada ya kumpokea Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, William Lukuvi, viongozi hao vyama wamesema siasa za mwaka 2019 namna uchaguzi ulivyoendeshwa madhila waliyopitia kuenguliwa wagombea wao bila sababu ya msingi waliona haina haja ya kupenda tena siasa na walikata tamaa.

Wamesema kupitia uongozi wa Rais Samia wa kuwaita na kukaa meza moja kufanya maridhiana kusahihisha makosa yaliyofanyika hivyo hawana budi kushiriki uchaguzi na wana imani ya kupata ushindi .

Mwenyekiti wa Chama cha Ukombozi UDP John Cheyo amesema wana imani na uongozi wa Rais Samia hivyo wanapenda kuona amani iliyopo ikidumu na wataendesha siasa zao kistaarabu bila kuleta mtafaruku wowote.

“Ni jambo jema vyama vyote vikajenga utu katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, hivyo wamejipanga kushiriki na wataweka wagombea wao kila mahali” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi CUF, Prof Ibrahim Lipumba amekiri kuwa kuona mabadiliko makubwa ya kisiasa licha ya matatizo madogomadogo falsafa ya 4R inafanya kazi hivyo wao ni wadau wa Diplomasia wanapenda haki itendeke na amani iendelee.

‘” Sisi chama chetu kimeona 4R za Rais Dkt Samia Suluhu kuleta maridhiano ya kisiasa Ustahimilivu haki hivyo tunakiri hata kuona kwa mara ya kwanza waziri aliyepewa dhamana na timu ya msajili wa vyama vya Siasa kutenga muda kututembelea ofisini kwetu na kutusikiliza maoni yetu tunapoelekea uchaguzi hili ni jambo la kihistoria Waziri Willium Lukuvi ameanzisha lisiishie hapa ” amesema Prof Lipumba.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha NLD Hassaan Doyo amesema chama chao hakina sera ya kususia uchaguzi licha ya kutokuwa na ruzuku na wana hali mbaya ya kuchumi wamekuwa wakiendesha chama hiko kwa fedha zao za mifukoni hivyo wanaomba Waziri amfikishie Dkt Samia Suluhu Hassan awafikirie hata nao waweze kuingia katika mtanange wa kinyang’anyiro cha uchaguzi wa Serikali za Mtaa wakiwa na hali nzuri wanapoendesha kampeni zao.

” Tunakupa pongezi Waziri Willium Lukuvi kwa kuaminiwa na Rais Dkt Rais Samia na bila ubaguzi umefanya ziara kututembelea kujua ofisi zetu zilipo na kusikiliza changamoto zetu zinazotukabili pamoja na kuchukua maoni kwenda kuyafanyia kazi” amesema Doyo.

Mara baada ya kusikiliza vyama vyote Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu sera bunge na Uratibu Willium Lukuvi amesema tamaduni za kiafrika mtu akifika nyumbani ana kakuheshimisha sana kuliko mkikutana njiani hivyo ziara yake anayoifanya inajenga mahusiano mazuri wanapoelekea uchaguzi.

Amesema Serikali inaheshimu sana vyama.vingine vya siasa na amewapongeza kwa.kuendesha siasa zao za upendo na namna walivyotoa shukrani zao zimfikie Rais Dkta Samia Suluhu Hassani nia yake ya kuimarisha 4R hivyo hoja zao zote walizozitoa ameahidi atamfikishia kwani ni Rais wa wote licha ya kutoka chama tawala.

Naye Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi amesema ziara iliyofanywa na Waziri Lukuvi inamanufaa mbalimbali ikiwemo kujua zilipo ofisi za vyama hivyo na kujenga mahusiano mazuri baina yao hata kama kuna jambo lolote linalotatiza wanauweza kukaa meza moja na kulitatua pasipo kufika katika majukwaa .