Vyama vya siasa 18 vyenye usajili wa kudumu vimeshiriki Katika kikao Cha kusaini kanuni za Maadili ya Uchaguzi wa Rais wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Mwaka huu huku chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikiwa hakina uwakilishi.
Kanuni hizo zinasainiwa na vyama vya Siasa vyenye usajili wa kudumu,Serikali na Tume ya Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC)
Vyama vilivyoshiriki ni Chama Cha Mapinduzi CCM, ACT wazalendo, Chama Cha Wananchi CUF, Chama Cha kijamii CCK, ADC, DP, Demikrasia Makini, NCCR Mageuzi , NLD, NRA, SAU, TLP, UDP, ADA TADEA, AAFP, CHAUMA, UMD na UPDP.
Aidha Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) hakikahudhuria hafla ya utiaji saini za Maadili.


