Rais wa Urusi Vladimir Putin ameibuka mshindi kuliongoza taifa hilo kwa muhula mwingine ujao wa miaka sita baada ya kujipatia ushindi mkubwa.Ushindi huo ulitarajiwa katika upigaji kura uliomalizika siku ya jumapili.Hata kabla ya kura zote kuhesabiwa tayatri alikuwa amejizolea asilimia 76 kwa mjibu wa tume ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa kutangazwa mshindi amsema ushindi wake ni matokeo ya hatua kubwa ya mafanikio aliyoyafikia katika uongozi wake.

Putin ameongeza kuwa hii ni uthibitisho wa kukubalika kwa sera zake na kwamba hana mpango wowote wa kufanya marekebisho ya katiba na kusisitiza umoja na mshikamano.

“Hadi hapa sina mpango wowote wa kufanya marekebisho yoyote ya katiba,kuhusiana na unyekiti na serikali kwa ujumla.Nilikwisha sema awali kwamba nafikiria suala hilo.Lakini kuanzia leo naanza kufikiria kwa undani,kwa sababu nilipaswa kusubiria matokeo ya uchaguzi kwanza.Mabadiliko yote yatatangazwa yakifuatiwa na uzinduzi..”

Akijibu maswali kutoka kwa waandishi wa habari Putin amekwepa swali alilotakiwa kueleza kama atagombea katika muhula ujao pia.

“Kwangu kile mnachotaka kuniuliza inakuwa kama mizaha Fulani hivi,hebu tuhesabu,ina maana nitasalia madarakani hadi nikiwa na miaka 100? Hapana hapana hapana. ”

Ushindi huu mkubwa ambao ulitarajiwa,umekuwa na ongezeko la kura ikilinganishwa na ushindi wa asilimia 64 mwaka 2012.Ambapo m,pinzani wa karibu wa Putin milionea Pavel Grudinin,yeye alipata asimilia 12.