Nchi 32 wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) zinatarajiwa kwenda nchini Urusi kushiriki michuano ya kombe la dunia, viwanja 11 vinavyotarajiwa kutumika nchini humo ni vifuatavyo
- Luzhniki Stadium, Moscow
Hiki ni kiwanja kikubwa kuliko vyote nchini humo na kinauwezo wa kuingiza watazamaji 81,006 walioketi kinatarajiwa kufunguliwa wakati wa mashindano hayo.
Kilijengwa mwaka 1956 na sasa kinafanyiwa ukarabati na kinatarajiwa kuwa tayari na kuwa tayari kutumika mwaka huu na kiwango cha juu cha joto ni 23 cha chini nyuzi joto 18, uwezekano wa kunyesha mvua ni asilimia 50.
- Spartak Stadium, Moscow
Huu nao ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika, uwanja huo umebalisbhwa jina siku chache zilizopita, awali ulikuwa ukiitwa Otkrytiye Arena una uwezo kuingiza watazamaji 43,298 na kilifunguliwa mwaka 2014.
Kiwango cha juu cha joto ni 23 na cha chini 18, uwezekano wa kunyesha mvua ni asilimia 50.
- Nizhny Novgorod Stadium, Nizhny Novgorod
Uwanja huu upo maili 265 mashariki mwa jiji la Moscow eneo ambalo huvutia kutokana na kuzungukwa na vitu vya asili na umbile lake ni duara huku ukiwa na taa za rangi mbalimbali nyakati za usiku una uwezo wa kuingiza watazamaji 45,331, kimefunguliwa rasmi mwaka huu.
Kiwango cha juu cha joto ni nyuzi joto 23 na cha chini 13, uwezekano wa kunyesha mvua wakati wa mashindano ni asilimia 60.
- Mordovia Arena, Saransk
Uwanja huu upo Kusini Mashariki mwa jiji la Moscow, umejengwa kwa rangi nyingi za kuvutia una uwezo wa kuingiza watazamaji walioketi 45,000, uwanja huo utafunguliwa rasmi wakati fainali hizi za Kombe la Dunia mwaka huu.
Kiwango cha juu cha joto ni nyuzi joto 23 na cha chini 12, uwezekano wa kunyesha mvua wakato wa mashindano ni asilimia 33.
- Kazan Arena, Kazan
Uwanja huu mara nyingi watu wengi huu fananisha na ule wa Wembley ulioko nchini Uingereza au ule wa klabu ya Arsenal wa Emirates una uwezo wa kuingiza watazamaji 45,000, uwanja huo ulinguliwa mwaka 2013.
- Samara Arena, Samara
Uwanja huu umeendelea kutengenezwa na upo umbali wa maili 655 kutoka jiji la Moscow ni uwanja wa kisasa unaotarajiwa kuwa na uwezo wa kuingiza watu wapatao 44,807 na ulifunguliwa mapema mwaka huu.
- Ekaterinburg Arena, Ekaterinburg
Uwanja upo nje kidogo ya jiji la Moscow ni wa kisasa wenye uwezo wa kuingiza watazamaji wapatao 35,696 walioketi vitini na kilifunguliwa mwaka 1953 .
- Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Hiki nacho ni kiwanja cha kisasa chenye uwezo wa kuingiza watazamaji wapatao 68,134 walioketi vitini na kilifunguliwa mwaka jana.
- Kaliningrad Stadium, Kaliningrad
Uwanja huu ni miongoni mwa viwanja vitakavyotumika wakati wa michuano ya kombe la dunia, una uwezo wa kuingiza watazamaji 35,212 walioketi, kimefunguliwa mapema mwaka huu.
- Volgograd Arena, Volgograd
Uwanja huu upo umbali wa maili 585 kutoka mji mkuu wa Moscow unauwezo wa kuingiza watazamaji wapatao 45,568 walioketi viti na umefunguliwa mapema mwaka huu.
- Fisht Stadium, Sochi
Uwanja huu upo pwani ya bahari nyeusi unauwezo wa kuingiza watazamaji wapatao 47,700 ulifunguliwa miaka mitano iliyopita.