Viongozi wakuu wa nchi za Ukanda wa Afrika Mashariki wamefanya juhudi kwa mara nyingine za kujaribu kuuleta amani mashariki mwa Kongo.
Viongozi hao waliokutana Jumamosi bado walishindwa kupiga hatua kufuatia kutokuwepo kwa rais wa Jamhuri ya Kidemorasia ya Kongo na kuondoka mapema kwa mwenzake wa Rwanda katika mkutano huo wa kilele wa kikanda wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Taarifa iliyosomwa mwishoni mwa mkutano huo wa faragha mjini Arusha ilisema tu kwamba kuna haja ya kuzijumuisha pamoja juhudi zote za kutafuta amani ya kudumu Mashariki mwa Kongo.
Rais Paul Kagame aliondoka muda mfupi baada ya mkutano huo lakini hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu kutoshiriki kwa Felix Tshisekedi.
Viongozi wengine walioshiriki mkutano huo ni pamoja na Salva Kiir wa Sudan,Samia Suluhu wa Tanzania,William Ruto wa Kenya,Yoweri Museveni wa Uganda na Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia.
777777777777777777777
ACHR
Israel imesema imefanikiwa kulizuia kombora kutoka Yemen
MAMLAKA ya ulinzi wa anga ya Israel imesema imefanikiwa kulizuia kombora ambalo limefyatuliwa kutoka Yemen.
Asubuhi ya mapema ya jana ving’ora vya mashambulizi ya anga vilisikika karibu na Tel Aviv na katika maeneo mengine. Tovuti ya habari ya Israel ynet iliripoti kuwa milio hiyo ilisababishwa na kombora la balestiki.
Na jeshi likasema lilizuiwa kabla ya kuingia katika ardhi ya Israel. Na wakati kila upande ukiwa katika makubaliano ya kusitisha mapigano, Hezbollah, mshirika wa Iran huko Lebanon, wanamgambo wa Houthi wa Yemen, ambao pia wanaungwa mkono na Iran wametishia kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya Israel.
Wanasema uungaji mkono wao unaendelea kwa Wapalestina katikaUkanda wa Gaza, ambapo Israel imekuwa ikiendesha vita dhidi ya wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas tangu shambulio la Oktoba 7, 2023 katika ardhi ya Isreal.