VIONGOZI wa dunia wamelaani shambulizi la makombora la Uris dhidi ya Ukraine siku ya Jumapili, moja ya mashambulizi mabaya zaidi katika miezi kadhaa, huku Rais wa Marekani Donald Trump akiliita “jambo baya” na “kosa.”
Viongozi wa dunia wamelaani vikali Urusi kwa shambulizi la makombora dhidi yamji wa Sumy, kaskazini mashariki mwa Ukraine, lililotokea Jumapili asubuhi na kuwaua watu wasiopungua 34 huku wengine zaidi ya 100 wakijeruhiwa. Hili ni mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi tangu kuanza kwa vita. Rais wa Marekani Donald Trump alilitaja tukio hilo kuwa ni “jambo la kutisha” na “kosa.”
Kwa mujibu wa mamlaka za Ukraine, makombora mawili ya masafa marefu yalilenga katikati mwa jiji hilo lililo karibu na mpaka wa Urusi. Shambulizi hilo lilijiri siku mbili tu baada ya mjumbe maalum wa rais wa Marekani, Steve Witkoff, kusafiri kwenda Urusi kukutana na Rais Vladimir Putin kwa lengo la kuendeleza juhudi za Trump kusitisha vita hivyo vya zaidi ya miaka mitatu.
“Nadhani lilikuwa tukio baya sana. Niliambiwa walifanya kosa. Lakini ni jambo la kutisha. Vita vyenyewe ni jambo la kutisha,” alisema Trump akiwa njiani kurejea Washington ndani ya ndege ya Air Force One.
Alipoulizwa afafanue alichomaanisha kwa kusema “kosa”, Trump alijibu: “Walifanya kosa… utakwenda kuwauliza wao,” bila kufafanua alikuwa anamaanisha nani hasa.
