Viongozi wa dini nchini Kenya wamewataka wanasiasa wanaolumbana kuafikia amani kufuatia ghasia iliyomalizika huku kanisa na majengo yaliyounganishwa na msikiti kushambuliwa jijini Nairobi.

Katika maandamano yaliyofanyika Siku ya Jumatatu, yaliyoitishwa na kiongozi wa upinzani Raila Odinga yalisababisha polisi kukabiliana na waandamanaji.

Na Shamba la aliyekuwa Rais Uhuru Kenyatta lililengwa na waporaji.

Wakizungumza katika mtaa wa Kibera jijini Nairobi kufuatia kuzuka kwa ghasia, wawakilishi wa imani za Kikristo, Kihindu na Kiislamu walikuwa na ujumbe kwa wanasiasa wa Kenya.

Aidha walimtaka Rais William Ruto na Bw Odinga kuwa na mazungumzo ya amani na kuwataka wanasiasa wote wa Kenya kuipa nchi yao kipaumbele .

Inafahamika wazi kuwa chanzo kikuu cha machafuko hayo ni uhasama mkubwa kati ya Bw Ruto, Bw Odinga na Bw Kenyatta.

Katika miongo miwili iliyopita uhusiano kati yao ulibadilika sana kwani jumuiya nyingi ziliundwa na kusambaratishwa.

Hata hivyo kama wanasiasa watachochea ghasia zaidi, kuna hatari kubwa ya machafuko makubwa nchini Kenya.