Wizara ya Katiba na sheria imevishauri vyombo vya Usalama kufanya kazi kwa kuzingatia misingi ya Utumishi na Utawala bora badala ya matumizi ya nguvu katika Kutekeleza majukumu yao ya usalama.
Kauli hiyo ameitoa mwansheria kutoka Jeshi la Polisi Tanzania ACP Nicolaus Mhagama wakati wa mafunzo ya Utoaji Elimu ya Uraia kwa vyombo vya Usalama ,watumishi idara mbalimbali pamoja na watendaji wilayani Tarime Mkoani mara.
Nicolaus alisema kama vyombo vya Usalama kupitia viongozi wake vitafanya kazi kwa kuzingatia Sheria Utawala Bora utaimarishwa kwa kiasi kikubwa kwa jamii inayowazunguka nahiyo itasaidia utekelezaji wa 4R za Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
“Wakati nazungumza na viongozi hawa wakamati ya Usalama kanda maalum ya tarime Rorya na Wilaya ambazo tumepita tumesisitiza wazingatie Sheria hasa kuepuka matumizi ya nguvu katika Kutekeleza majukumu yenu maana mnafanya kazi kwa mujibu wa Sheria ya nchi”Alisema Nicolaus Mhagama mwansheria.
Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Tarime Meja Edward Gowele alisema Mafunzo hayo sasa yataongeza tija katika kufanya kazi.
“Niwaombe Sana twende kufanya kazi kwa kuzingatia Utawala Bora kila moja hapa nikiongozi anawatu anao wasimamia wanahitaji kukumbushwa mfano tunao askari wetu wanafanya kazi kwa Muda wote tuwakumbushe Utawala bora hasa linapokuja swala la ukamataji”Alisema meja Edward Gowele Mkuu wa Wilaya ya Tarime.
Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rorya DK Khalfan Haule ameishukuru Wizara ya Katiba na Sheria kuja na mafunzo hayo ambapo ameomba Elimu hiyo kupelekwa kwa viongozi wa chini wakiwemo wenyeviti wa Vijiji ambao ndio wakakaa na wananchi.