Tanzania imeendelea kujiongezea idadi ya vivutio vya kitalii baada ya Uwanja wa Taifa kuingia
katika kundi la viwanja 10 bora barani Afrika, vilivyojengwa kwa gharama kubwa na vyenye
ahadhi.
10- Uwanja wa Taifa Dar es Salaam: Uwanja ulijengwa kwa dola milioni 53 na nusu ya fedha
za ujenzi huo zilitolewa msaada na serikali ya China. ulifunguliwa mwaka 2007 na una uwezo
wa kuchukua mashabiki 60,000.
9- Stade Olympique de Radès: Huu ni uwanja nchini Tunisia mji wa Rades, una uwezo wake
wa kuchukua mashabiki sawa na uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ila gharama yake inatajwa
kufikia dola milioni 110, ulijengwa mwaka 2001.
8-Mbombela Stadium ni moja ya viwanja vilivyotumika katika fainali za michuano ya Kombe la
Dunia 2010 nchini Afrika ya Kusini, una thamani ya dola milioni 140, una uwezo wa kuchukua
mashabiki 40,929.
7- Peter Mokaba Stadium: Huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa ajili ya fainali za Kombe la
Dunia 2010 Afrika Kusini, ulijengwa kwa dola milioni 150 na una uwezo wa kuchukua
mashabiki 41,733, kwa sasa unatumiwa na klabu ya Black Leopards FC kama uwanja wa
nyumbani.
6- Estádio 11 de Novembro: Upo Angola lakini ulitumika kwa michuano ya Kombe la Mataifa
ya Afrika 2010, umejengwa kwa dola milioni 227 na una uwezo wa kuchukua mashabiki 50,000.
5- Nelson Mandela Bay Stadium: Huu ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 270, upo
katika mji wa Port Elizabeth na una uwezo wa kubeba mashabiki 48,459. Jina lake limetoka na
Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.
4- Abuja Stadium: Hiki ni moja kati ya viwanja vilivyojengwa kwa gharama zaidi barani Afrika,
dola milioni 360 ndiyo zilitumika kujenga uwanja huu wenye uwezo wa kuchukua mashabiki
60,491, upo mji mkuu wa Nigeria, Abuja.
3- FNB Stadium: Ni uwanja ambao ulijengwa kwa dola milioni 440, ulichezewa fainali za
Kombe la Dunia 2010 Afrika Kusini. FNB Stadium jina lake lilizoeleka na wengi ni Soccer City.
Huu ndiyo uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki wengi zaidi barani Afrika, una uwezo
wa kubeba watu 94,736.
2-Moses Mabhida Stadium ulijengwa kwa dola milioni 450, uwanja huu upo Durban, Afrika
Kusini na ulitumika kwa baadhi ya mechi za fainali ya Kombe la Dunia 2010, una uwezo wa
kuingia mashabiki 62,760 wakati wa fainali za Kombe la Dunia ulipunguzwa na kuwa na uwezo
wa kuchukua mashabiki 54,000.
1-Cape Town Stadium: Uwanja huu ndiyo uwanja wenye thamani kuliko vyote barani Afrika,
kwani zimetumika dola milioni 600, una uwezo wa kuingia mashabiki 64,100.