Waokoaji wamemuokoa mwanamke mmoja aliyefunikwa na kifusi kwenye jango la hoteli moja lililoporomoka nchini Myanmar, maafisa walisema siku ya Jumatatu.

Mwanamke huyo amekaa siku tatu baada ya tetemeko kubwa la ardhi lililosababisha vifo vya watu karibia 2,000 huku waokoaji nchini Myanmar na Thailand wakiendeslea kutafuta manusura zaidi.

Mwanamke huyo alitolewa kwenye vifusi baada ya saa 60 kukwama chini ya Hoteli ya Great Wall iliyoporomoka katika jiji la Mandalay baada ya operesheni ya saa 5 ya timu za waokoaji kutoka China, Urusi na wenyeji, kulingana na chapisho la ubalozi wa China kwenye Facebook. Ilisema alikuwa katika hali nzuri mapema Jumatatu.

Mandalay iilipigwa na tetemeko la ardhi la kipimo cha 7.7 siku ya Ijumaa ambalo lilisababisha uharibifu mkubwa nchini Myanmar na uharibifu katika nchi jirani ya Thailand.

Huko Bangkok, mji mkuu wa Thailand, wafanyakazi wa dharura wanaotumia mbwa siku ya Jumatatu waliendelea na msako mkali wa kuwatafuta watu 76 wanaoaminika kufukiwa chini ya vifusi vya jumba kubwa lililoporomoka.