Zikiwa zimesalia siku chache michano ya kombe la Dunia ianze kutimua vumbi huko mashariki ya kati, unaweza ukawa unavuta picha michuano ya msimu huu itakuwaje!
Hivi ndivyo viwanja nane ambavyo michuano hiyo itachezewa hapo nchini Qatar kuanzia Novemba 20, 2022
1. Uwanja wa Al Bayt
Uwanja huu upo jjini Al Khor ukiwa ni wa pili kwa ukubwa, unauwezo wa kubeba mashabiki 60,000 na hapa ndipo utakatwa utepe kwa mechi ya ufunguzi wa Kundi A kati ya Qatar dhidi ya Ecuador
2. Uwanja Lusail Iconic
Uwanja huu upo jijini Lusail na ndio uwanja mkubwa zaidi ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki mpaka 80,000 na hapa ndipo Fainali za kombe zitafanyikia.
3. Uwanja Ahmad Bin Ali
Uwanja huu unauwezo wa kubeba idadi ya mashabiki wapatao 40,000 na upo mjini Umm Al Afaei
4. Uwanja AI Janoub
Uwanja huu una muonekano wa kipekee na umejengwa kwa ufundi wa aina yake ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki wapatao 40,000 na unapatikana katika jiji la Al Wakrah
5.Uwanja Al Thumama
Uwanja huu wenye usanifu wa kipekee unaosadifu umbo la barghashia na utamaduni wa watu wa mashariki ya kati upo katika mji wa Al Thumama na una uwezo wa kubeba mashabiki 40,000 kwa mpigo.
6. Uwanja Education City
Uwanja huu upo Al Rayyan na unauwezo wa kubebe mpaka mashabiki 40,000
7. Uwanja Khalifa International
Huu unabebe mashabiki 40,000 na unapatikana katika mji wa Aspire
8. Uwanja 974
Uwanja huu ni wa aina yake na umejengwa kwa makontena chakavu 974 ambayo namba hiyo pia ndiyo Code ya nchi ukiwa na uwezo wa kubeba mashabiki 40,000, uwanja huu unahamishika na huenda mashabiki wakawa wanafurahia upepo wa bahari kutokana uwanja huo kuwa mita chache kutoka usawa wa bahari mjini Ras Abu Aboud .