Rais Paul Kagame ametumia uwezo wake kuwaachilia zaidi ya wafungwa 2000 waliokuwa wamefungwa kwa makosa kadhaa ya uhalifu.

Miongoni mwa wafungwa hao waliofaidika na hatua ya rais huyo ni mwanamuziki Kizito Mihigo ambaye alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 10 na Victoire Ingabire ambaye alikuwa katika kizuizi tangu 2010.

Victoire Ingabire alikuwa akihudumia kifungo cha miaka 15 kwa kutishia usalama wa serikali na kudunisha mauaji ya halaiki ya mwaka 1994.

Amekuwa akiongoza ukosoaji wa rais Paul Kagame huku akiongezea kuwa hukumu yake ilishinikizwa kisiasa.

Bi Ingabire

Bwana Kagame amepongezwa kwa kurekebisha uchumi wa Rwanda lakini pia ameshutumiwa kwa ukiukaji wa haki za kibinaadamu.

Kuwachiliwa huru kwa bi Ingabire na wafungwa wengine 2,140 kulitangazwa na seriikali kufuatia mkutano wa baraza la mawazitri.

Taarifa ilisema kuwa bwana kagame aliwaonea huruma chini ya uwezo wake kama raia.

Mbali na Ingabire ni mwanamuziki Kizito Mihigo mbaye alifungwa kwa miaka 10 2015 kwa kupanga njama za kumuua rais Paul kagame.

Mwanamuziki Kizito Mihigo baada ya kuachiliwa
Kizito Mihigo

Alipokuwa akitoka jela, bi Ingabire alimshukuru rais kagame, akisema huu ndio mwanazo wa kufunguka kwa sehemu ya kisiasa nchini Rwanda, kulingana bna shoirika la AFP.

Lakini waziri wa haki Johnston Businge alipuuzilia mbali umuhimu wa kuachiliwa kwa bi Ingabire.

Hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kuachiliwa kwake-na hakuna chochote cha kisiasa kuhusu kufungwa kwake, aliambia Reuters.

Lakini Je Ingabire ni nani?

Boi Ingabire alirudi kutoka jela nchini Uholanzi 2010 ili kushiriki katika uchaguzi wa urais.

Alikamatwa na kuzuiliwa kuwania urais na amekukuwa akihudumia kifungo jela tangu wakati huo.

Bi Ingabire , ambayte ni mwanachama wa kabila la Hutu, alikuwa akihoji ni kwa nini makumbusho ya mauaji ya halaiji nchini Rwanda ya 19914 hayakuhusisha watu wa kabila la Hutu.

Wengi ya watu 800,000waliouawa walikuwa wala la Tuts lakini Wahutu wenye msimamia wa kadri pia waliuawa na wahutu wenye msimamo mkali.

Chama cha Rwanda patriotic Front cha Rais Kagame kinachotawaliwa na Watutsi wengi kilimaliza mauaji hayo.