Na Dotto Kwilasa, JamhuriMedia,Dodoma

WAZIRI wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Aldof Mkenda, ametangaza kwamba mkutano wa uzinduzi wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, toleo la 2023, sasa utafanyika Februari 1, 2025, badala ya Januari 31, 2025, kutokana na sababu zisizoweza kuzuuilika.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Januari 30, Prof. Mkenda alifafanua kwamba mgeni rasmi katika mkutano huo atabaki kuwa Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia anatarajia kuona vijana wa Kitanzania wakipata maarifa na ujuzi wa kutosha ili kukabiliana na changamoto za maisha na kuchangia maendeleo ya taifa.

Aidha, Waziri Mkenda alisisitiza kuwa maandalizi ya sera na mkakati wa utekelezaji wake yamekamilika, akiongeza kuwa lengo ni kuandaa wanafunzi kuwa mahiri katika kukabiliana na mahitaji ya dunia ya sasa.