MAMBO ni fire katika Uwanja wa Taifa ambapo tayari mashabiki, wapenzi wa soka wameshaanza kuingia uwanjani kushuhudia mtanange kati ya Timu ya Simba na Kagera Sugar huku wafanyabiashara wadogo wadogo nao wanaendelea kuuza jezi za Simba nje ya uwanja huo kama kawaida.
Askari wa kutuliza ghasia wamejaa wakilinda amani eneo la nje na ndani ya uwanja ili kuhakikisha mambo yote yanakwenda kama yalivyopangwa katika zoezi la Kihistoria ambapo Simba watakabidhiwa Kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (VPL) kwa msimu wa 2017/2018.
Katika malango ya Uwanja huo, tiketi zinaendelea kuuzwa kwa kasi huku biashara nyingine ndogondogo zikiendelea pia.
Rais Dkt. John Magufuli ndiye anatarajiwa kutawakabidhi Simba kombe hilo Simba ambao wanafikisha Ubingwa wa 19 wa ligi hiyo huku watani waoambao ni mabingwa watetezi, Yanga wameshanyakua maranyingi zaidi wakichukua mara 27.
Rais Magufuli leo ataungana na wanamichezo kupokea Kombe la Ubingwa wa CECAFA kutoka Timu ya Serengeti Boys, kuipokea timu ya TSC iliyoibuka washindi wa pili wa Dunia huko Urusi na kukabidhi kombe kwa Mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Uwanja wa Taifa Dar, kuanzia saa 8 mchana.