Uturuki yasema itakuwa kosa kujaribu kueleza kuwa matukio ya Syria yametokana na uingiliaji wa mataifa ya kigeni.

Uturuki, ambayo inaunga mkono makundi ya waasi nchini Syria, imetupilia mbali wazo lolote la kwamba vurugu za kaskazini mwa Syria zimetokana na uingiliaji wa nchi za kigeni.

” Tumebadilishana maoni yetu kuhusu matukio ya hivi punde nchini Syria na viongozi wenzangu. Kwa sasa, itakuwa kosa kujaribu kueleza kuwa matukio ya Syria yametokana na uingiliaji wa mataifa ya kigeni.

Hili ni kosa ambalo hutumiwa na wale ambao hawataki kuelewa hali halisi ya Syria.”

Waziri huyo wa mambo ya Nje wa Uturuki amesema serikali ya Rais Bashar al-Assad inapaswa kuanzisha mazungumzo na makundi ya upinzani.

Jeshi la Syria likisaidiwa na vikosi vya Urusi vinaendelea kukabiliana na waasi hao ambao wamechukua udhibiti wa mji wa Aleppo. Watetezi wa haki za binaadamu wamesema operesheni hiyo imesababisha vifo vya watu 11, wakiwemo watoto.