Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
Imeelezwa kuwa uwepo wa biashara haramu ya viumbe pori una athari mbalimbali katika maeneo ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.
Hayo yamebainishwa Mkuu wa Kitengo cha Sera na Usimamizi mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili, Allen Mgaza Mgaza ameyasema hayo jana juzi kwenye mdahalo maalum ulioandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kwa ufadhili wa USAID kupitia mradi wake wa USAID Tuhifadhi Maliasili.
Mdahalo huo ulioshirikisha Waandishi wa Habari za Mazingira ulioneshwa moja kwa moja na shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kupitia chaneli yake ya Safari.
Amesema kuwa kutokana na jitihada za wadau katika kukabiliana na biashara hiyo, Serikali imewapongezwa kwa jitihada kwa hatua wanazozichukua katika kukabiliana na biashara haramu ya viumbe pori.
“Biashara haramu ya viumbe pori ni miongoni mwa biashara haramu kubwa zinazotikisa duniani ikishika nafasi ya nne huku Dawa za kulevya, bidhaa bandia na usafirishaji wa Binadamu zikitajwa kuongoza kwenye mlolongo wa biashara haramu duniani.
“Uwepo wa biashara haramu ya viumbe pori unaathiri maeneo mbalimbali katika eneo la kiuchumi, kijamii na kimazingira hivyo kutokana na jitihada kubwa wanazozifanya wadau katika kukabiliana na biashara serikali imetoa pongezi,” amesema.
Ameongeza kuwa bila ushiriki wa pamoja haitakuwa rahisi kupambana na biashara hiyo, badala yake uhalifu huo utaendelea.
Amesema biashara haramu ya viumbe pori ni tatizo na ili kukabiliana nalo ni lazima kuwe na juhudi za pamoja kitaifa na kimataifa, wizara na taasisi za serikali, sekta binafsi na hata mtu mmoja mmoja, wote wanapaswa kushiriki katika kupambana na biashara hii haramu ya viumbe pori.