Wizara ya Ulinzi ya Urusi inadai kuwa ndege zisizo na rubani 22 za Ukraine zilidunguliwa katika maeneo sita ya Urusi usiku kucha, ikiwa ni pamoja na yale yaliyo mbali na mipaka ya Ukraine.

Ujumbe mfupi kutoka kwenye mitandao ya kijamii ya wizara hiyo unasema kuwa ndege 10 zisizo na rubani zilidunguliwa katika eneo la Bryansk, nne kila moja katika mikoa ya Oryol na Rostov, mbili katika mkoa wa Belgorod, na droni moja kila moja katika mikoa ya Volgograd na Lipetsk.

Huku hayo yakijiri, Katika mji mkuu Kyiv, nyumba ya kibinafsi iliwaka moto baada ya na kuangukiwa na uchafu kutoka kwa droni iliyoungua.

Kulingana na mkuu mpya wa utawala wa kijeshi wa Kyiv, Timur Tkachenko, moto huo uliozuka katika wilaya ya Darnitsky kusini mashariki mwa mji mkuu, tayari umezimwa.

“Waokoaji walizima moto, habari kuhusu waathiriwa wa tukio hilo bado hazijatolewa.”

Ndege nyingine isiyo na rubani ya kamikaze ya Urusi ilitunguliwa kwenye wilaya ya Goloseevsky kusini mwa Kyiv, kulingana na meya wa Kyiv Vitaliy Klitschko.