Urusi imetangaza kuzifungia vyombo vya habari 81 vya Ulaya kutangaza kwenye ardhi ya yake.

Katika taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Urusi iliyotolewa Jumanne orodha hiyo inajumuisha vituo 77 vya habari, magazeti, majarida na machapisho ya mtandaoni kutoka nchi 25 za Umoja wa Ulaya.

Wizara ya Mambo ya Nje inasema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na uamuzi wa Umoja wa Ulaya ulioanza kutekelezwa leo wa kupiga marufuku RIA Novosti, Izvestia na Rossiyskaya Gazeta kutoka katika maeneo ya Umoja wa Ulaya.

Vyombo vya habari vya Latvia, Televisheni ya Latvia na Redio 4 ya Latvia vinazotangaza kwa lugha ya Kirusi, pamoja na gazeti la Diena, tovuti ya mtandao apollo.lv na chaneli ya TV ya mtandao tvnet.lv vimefungiwa.

Estonia: Shirika la utangazaji la umma la ERR, chapisho la mtandaoni la Delfi.ee na tovuti ya propastop.org zimefungiwa nchini Urusi.

Luthuania, tovuti ya shirika la utangazaji la umma, ambayo inafahamika kama “LRT Internet portal,” na mitandao mingine miwili ya habari imepegwa marufuku.

Finland: Kampuni kubwa ya televisheni na redio ya nchi hiyo Yle na magazeti matatu maarufu yalifungiwa Urusi.

Tangu mwanzo wa vita, mamlaka za Urusi imefungia vyombo vya habari, ikiwa ni pamoja na BBC Idhaa ya Kirusi.