Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema leo kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga imezidungua droni 47 zilizorushwa na Ukraine katika mashambulizi yaliyolenga miji mitano na ambayo yamewajeruhi watu sita.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema leo kwamba mifumo yake ya ulinzi wa anga imezidungua droni 47 zilizorushwa na Ukraine katika mashambulizi yaliyolenga miji mitano na ambayo yamewajeruhi watu sita.
Gavana wa mkoa wa Rostov, Yuri Sliusar amesema katika shambulio lililolenga mji wake huo limeharibu nyumba kadhaa na kujeruhi watu wawili.
Upande mwingine, Ukraine nayo imeripoti kuzidungua droni 100 kati ya 179 zilizorushwa na Urusi katika mashambulizi ya usiku wa kuamkia leo Jumamosi.
Jeshi la anga la Ukraine limeongeza kwamba droni zingine 63 zilipotezwa mwelekeo ingawa uharibifu umeripotiwa katika maeneo ya miji ya Zaporizhzhia, Kharkiv, Sumy na Kyiv.
Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi ya anga wakati ambapo rais wa Marekani Donald Trump akiishinikiza Urusi kukubaliana na Ukraine katika mpango wa usitishaji wa vita hivyo vinavyoendelea kwa zaidi ya miaka mitatu sasa.