Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Songea

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), limekamilisha safu ya uongozi wa Kamati ya Utendaji (KUT), baada ya kupatikana mwenyekiti, Makamu mwenyekiti pamoja na wajumbe saba wa kamati tendaji.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Frank Sanga, alisema wajumbe wa mkutano walikuwa 153 ambapo alisema Mwenyekiti Deodatus Balile na Makamu wake,Bakari Machumu wamepita bila kupingwa baada ya kuwa wagombea pekee wa nafasi hizo.

Hatua hiyo ni kutokana kulikosekana pingamizi kwa mujibu wa kanuni, jambo linaloipa mamlaka kamati kuwatangaza wagombea pekee kuwa washindi wa nafasi hizo.

Sanga alisema kwa nafasi ya ukumbe kulikuwana wagombea 12 ambapo wagombea saba pekee ndio wanahitahija ambapo

Sanga alisema kwa mujibu wa sheria na kanuni za TEF, Balile ameshinda kwa kuwa alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na hakuna wa wapig kura waliopinga nafasi hiyo.

Kwa wa sheria na kanuni za uchaguzi wa jukwa hilo endapo mgombea mmoja atajitokeza kwa nafasi yeyote ya hizo atachahuliwa moja kwa moja isipokuwa wanachama watakapoweka pingamizi.

Pia kwa mujibi wa sheria na kanuni za TEF namba 7 na 8, Machumu ameshinda kwa. Kuwa alikuwa mgombea pekee wa nafasi hiyo na hakukuwa na wapigakura waliopinga.

Waliochaguliwa kuwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji TEF, Bakari Kimwaga (114), Salim Salimi (108 ), Joseph Kulangwa (107) na Stella Aron (99), Caren Taus Mbowe (98), Anna Mwasyoke (83) na Jane Mihanji (73)

Wagombea wengine walikuwa Peter Nyanje(72), Yasin Sadick (60), Reginald Miruko (49), Esther Zelamula (39) na Angelina Akilimali (32)