Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuunga mkono la kisheria la Palestina linaloitaka Israel kuondoka Gaza na maeneo yanayokaliwa kwa mabavu katika ukanda wa magharibi nchini humo.
Mataifa 43 kati 193 zikiwemo Ujerumani, yamejizuwia kupiga kura kuhusu azimio hilo lililowasilishwa katika kikao hicho cha Umoja wa Mataifa.
Wengine ambao waliopiga kura za hapana ni Israel na Marekani dhidi ya rasimu ya azimio hilo pamoja na mataifa mengine 12, huku baadhi ya mataifa mengine yaliyobaki yakishindwa kupiga kura.
“Hivi ndivyo siasa za kijinga za kimataifa zinavyoonekana,” msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Israel Oren Marmorstein alisema kwenye mtandao wa X baada ya nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kupitisha maandishi ya azimio hilo kwa kura 124 dhidi ya 14 huku wanachama 43 wakijizuia”.
Alisema ni “uamuzi potofu ambao umetenganishwa na ukweli, unahimiza ugaidi na unahamasisha fursa za amani”.