Nchi za NATO barani Ulaya ziliongeza zaidi ya maradufu uagizaji wa silaha huku ikinunua zaidi ya asilimia 60 ya silaha za Marekani, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti na Amani (SIPRI).
Nchi za Ulaya zilizomo kwenye Jumuiya ya NATO ziliongeza zaidi ya maradufu uagizaji wa silaha katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, huku ikinunua zaidi ya asilimia 60 ya silaha kutoka nchini Marekani, hii ikiwa ni kulingana na ripoti ya Taasisi ya Kimataifa ya Utafiti wa Amani ya Stockholm (SIPRI) hii leo.
Matokeo haya ya SIPRI yanakwenda sambamba na tangazo la Umoja wa Ulaya kwamba wanakusudia kuimarisha uwezo wa kiulinzi wa bara hilo ili kukabiliana na mabadiliko ya sera za kigeni za Marekani chini ya Rais Donald Trump.
Ripoti hiyo inaitaja Ukraine kuwa muagizaji mkubwa zaidi wa silaha duniani katika kipindi cha 2020 hadi 2024.
Marekani ilisalia kama muuzaji mkubwa wa silaha duniani, kwa mauzo ya nje yaliyofikia asilimia 43, ikifuatiwa na Ufaransa, iliyouza kwa asilimia 9.6
