Vyanzo vya BBC katika Idara za Usalama za Ukraine vinadai kuwa Ukraine ndio imehusika na operesheni ya kumuua Igor Kirillov mjini Moscow.
Kulingana na chanzo hicho, pikipiki iliyokuwa na vilipuzi ililipuliwa wakati Kirillov na msaidizi wake wakikaribia jengo moja huko Moscow asubuhi ya leo.
Chanzo hicho kinadai Kirillov ni “mlengwa halali” kwa vile alikuwa mhalifu wa kivita ambaye alitoa amri ya kutumia silaha za kemikali zilizopigwa marufuku dhidi ya jeshi la Ukraine.
Luteni Jenerali Kirillov alikuwa akisimamia vikosi vya ulinzi vya nyuklia vya Urusi – Vikosi vya Ulinzi vya Nyuklia, Baiolojia na Kemikali.