Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema usiku wa kuamkia Ijumaa imefanikiwa kudhibiti mashumbulizi ya droni za Ukraine ambapo imezidungua na kuziteketeza droni 121 ambazo zilikusudiwa kuilenga mikoa 13, ikiwemo Moscow.

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema usiku wa kuamkia Ijumaa imefanikiwa kudhibiti mashumbulizi ya droni za Ukraine ambapo imezidungua na kuziteketeza droni 121 ambazo zilikusudiwa kuilenga mikoa 13, ikiwemo Moscow.

Pamoja na nguvu kubwa ya mashambulizi hayo lakini wizara hiyo haijazungumza chochote kuhusu athari zake. Lakini wizara imesema droni sita zimeharibiwa kwenye  mkoa wa Moscow na nyingine katika eneo la jiji haswa, na nyingine zililenga mikoa mingine, ikiwa ni pamoja na ile inayopakana Ukraine na Kursk, ambapo askari wa Ukraine wanadhibiti eneo la ardhi licha ya juhudi za Urusi kuwaondoa.

Aidha wizara hiyo ilisema droni nyingine 20 pia zililenga eneo la Ryazan, kusini mashariki ya Moscow, ambapo taswira za matukio ambazo hazikuweza kuthibitishwa mara moja zilichapishwa katika mitandao ya kijamii. Kunaonekana moto mkubwa katika jiji hilo kadhalika kituo cha mafuta na cha umeme kimeshambuliwa.

Wakati huo huo, jeshi la anga la Ukraine limesema limefanikiwa kudibiti shambulizi la Urusi la droni 25 kati ya 58 zilizorushwa usiku wa kuamkia leo. Wizara ya mambo ya ndani ya Ukraine imesema mashambulizi hayo yamewaua wanaume wawili na mwanamke katika mkoa wa kati wa Kyiv, na kwamba mtu mwingine amejeruhiwa.