Na Pendo Nguka, JamhuriMedia, Dar es Salam

Ukosekanaji wa umeme wa kutosha hupunguza pato la Taifa (GDP) kwa asilimia 2 hadi 4 kwa kila mwaka.Upatikanaji wa umeme ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Afrika.

Hayo yameelezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dkt.Akinumwi Adesia wakati akizungumza katika Mkutano wa Nishati wa wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea jijini Dar es salaam.

“Sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti ndio maana mimi pamoja na Ajay Banga Rais wa Benki ya Dunia tulishirikiana kuzindua M300 lengo likuwa ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 ifikapo 2030”

Aidha ameeleza kuwa Mission 300 imekuwa ni harakati ya kitaifa hivyo tukiungwa mkono na tume ya umoja wa Afrika na washirika mbalimbali wa kimataifa wakiwemo Rockefeller foundation, Sustainable energy for All ya umoja wa mataifa na Global Alliance energy for people and the planet ili kuharakisha matumizi ya Nishati safi.

Hatuko peke yetu katika kufanikisha mradi huu tumeungwa mkono na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu , Benki ya Miundombinu ya Asia , Shirika la Maendeleo ya Ufaransa pamoja na mashirika mengine ya maendeleo ili kufanikisha mpango huu.