Kampuni ya SABmiller haitafuni kwa bahati mbaya matunda ya kodi pekee kutoka nchi zinazoendelea.
Mikakati yake ya kukwepa kodi ni zaidi ya kawaida, kwani inatumia njia ya kampuni zinazohusiana na kampuni hiyo zilizozoko sehemu mbalimbali duniani.
Kadhalika, inatumia Kundi la Mawaziri wa Fedha 20 na Magavana wa Benki Kuu (linalojulikana kama G-20 na pia G20 au Group of Twenty) pamoja na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo (OECD), kutoka nchi zenye uchumi mkubwa duniani kujadiliana namna ya kukwepa kodi na kukimbilia mahali salama bila kugundulika.
Lakini kwa hali ilivyo sasa nchi zinazoendelea ndizo zinazoumia kwa kupoteza mapato mengi. Mtazamo wa ActionAid kwa hali ilivyo sasa ni kutaka mabadiliko ya haraka ili kubadili upepo wa kiuchumi.
Njia inayotumia SABmiller kukwepa kodi
Kampuni ya SABmiller inaundwa na zaidi ya kampuni tanzu 465 zilizo katika nchi 67 huku ikiwa na washirika na wadau wengine. Miongoni mwa kampuni hizo ni pamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL).
Si kampuni tanzu zote zinazohusika katika uzalishaji, masoko na kusambaza bia, bali nyingine zipo kwa ajili ya kusimamia na kusaidia kampuni ili kuhakikisha tu kwamba maslahi ya SABmiller hayapotei.
Ndani yake kuna mameneja kwa ajili ya kufanya kazi hiyo tu. Nyingine zipo kwa ajili ya kushikilia mali za kampuni, kwa mfano, kusimamia nembo ya biashara na kulinda ubunifu wa mali. Miundo hiyo inasaidia sana kampuni kusimamia, kulinda na kuendesha mali zake kwa ufanisi.
Lengo kuu ni kubaki na mafanikio. SABmiller ina kampuni angalau 65 za kuweka mambo sawa, mbali ya zile zinazozalisha bia na kutengeneza chupa karibu katika nchi zote za Afrika zinazofikia 64.
Ndani yake kuna kampuni 17 za Kidachi zinazojishughulisha na masuala ya uhasibu, Mauritius kuna kampuni 11, kampuni nane ziko Uingereza kwenye Visiwa vya Virgin, sita Uswisi na nyingine sita ambazo zinaitegemea Uingereza kama taifa kiongozi.
Hapana shaka kutakuwa na sababu za kutosha za kibiashara za SABmiller kuwa na kampuni tanzu nyingi zilizotawanywa sehemu mbalimbali duniani, katika dhana tu ya kupata nguvu ya kusimamia mali zake.
Uthibitisho upo kwenye ripoti na matokeo ya kufanya hivyo ni wajibu wa SABmiller wenyewe kwa namna inavyoweza kuchuma kodi nyingi.
SABmiller wenyewe wanathibitisha kwa kusema: “Mkakati ni kusimamia kodi zote bila kutetereka au kutoka nje ya ushindani kwa misukosuko yoyote.”
Mwaka 2010 SABmiller ilipata mshtuko kwa anguko katika ukusanyaji wa kodi ambako pamoja na sababu nyingine, ilithibitishwa kuwa sababu nyingine zilikuwa ni zaidi ya kupishana mawasiliano na hasa utozwaji tofauti wa kodi katika mataifa mbalimbali na mabadiliko ya vipimo vya kodi.
Uamuzi wa hivi karibuni uliotangazwa na Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kituo cha Televisheni cha Sky News, Graham Mackay, unathibitisha pasi shaka kwamba kitendo kinachofanywa na SABmiller ni kama mpango maalumu kuwa na matawi mengi.
“Kitu kimoja kinachofanywa na SABmiller ni kuhamishia makao makuu yake London na kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa la London mwaka 1999 ilikuwa ni namna ya kujiweka huru … kwa sababu kodi ni sehemu muhimu ya kuamua kujipambanua kibiashara nje ya mipaka na si kujibana kwenye kamji kama Ukbut huko Zug, Uswisi,” alisema Mackay.
SABmiller imesema kwamba nukuu hiyo ya Mackay inazungumza vipato vya mtu mmoja mmoja, baada ya waajiriwa kulipwa mbali ya kuwajibika kwa kampuni ingawa anayefaidika na mpango huo atakuwa yuko Uswisi.
Sky News imefanya tathmini yake na kuona kwamba kuanzishwa kwa mpango huo wa SABmiller wa kupata kodi tulivu, unagharimu ajira za watu wanaofikia 400.
Msimamo wa maendeleo wa SABmiller unasema: “Maendeleo endelevu yanahitaji kuwa sehemu ya kila tunachokifanya kila siku. Haina budi kuunganishwa na kufanya uamuzi katika kuendesha biashara.”
Ili kuthibitisha hili, SABmiller imetenga kampuni nne miongoni mwa kampuni zake kupata kipaumbele cha kufanyiwa mabadiliko ya kuhakikisha zinakuza faida zao katika biashara na kudumu katika biashara hizo.”
SABmiller imelichukua hilo kama wajibu wake na kutekeleza dhamira yake ya kuleta maendeleo na kujiboreshea faida katika mpangokazi wa miaka 10 ijayo, ambako imeegemea katika uzalishaji wa vinywaji vyake ikiwa ni pamoja na kupunguza kiwango cha maji na kuunga mkono shughuli za maendeleo ya jamii. Na hiyo ni katika dunia nzima.
Hilo la jamii lilionekana kupewa kipaumbele wakati timu ya ActionAid ilipofanya ziara jijini Accra, Ghana ambako pamoja na mambo mengine wataalamu hao walitembelea kiwanda cha bia.
Si kawaida ya SABmiller kutangaza faida zake kwa uwazi hasa katika wake mpangokazi wa miaka 10 kwa kila kampuni ambayo inaiendesha kwa njia ya mtandao.
Katika sekta ya maji, kwa mfano, SABmiller inashirikiana na Mfuko wa Dunia wa Majiasili (WWF) ili kukadiria matumizi badala ya matumizi ya ziada.
Mfuko huo unasema kwamba SABmiller “wameonesha uelewa mpana katika suala la maji kwamba ni taasisi chache zinazoweza kukubaliana na hali hiyo na kuthibitisha .”
Katika kupiga hatua za maendeleo, SABmiller imejiingiza kwenye jamii na kutumia zaidi ya pauni milioni moja huko Sudan Kusini kujenga mtandao wa wakulima wadogo wanaofikia 5,500. Wakulima hao huzalisha mihogo kama zao mbadala la kuzalisha bia.
Katika tawi lake la Afrika Kusini ambako SABmiller imeweka ngome ya programu ya kuboresha na kuwezesha uchumi wa watu weusi, matokeo yanaonesha kwamba wadau wapya 40,000 katika kampuni zake tanzu za Afrika Kusini, zimegawanywa na kuingizwa kwenye kundi la SAB Ltd, na kihistoria inaonesha ni waajiriwa wasio na faida.
“Kwa mbali mchango mkubwa katika biashara unaoweza kutengeneza maendeleo ya haraka ni namna ambavyo biashara hiyo itaendeshwa – kulipa waleta bidhaa, kulipa mishahara na kulipa kodi,” anasema Makay.
Kitengo cha Uchumi cha SABmiller kimesema kimelipa kodi ya kampuni zake duniani dola za Marekani bilioni 4.445 kwa mwaka wa fedha 2009-10.
Kiasi kikubwa cha kodi hiyo (dola za Marekani bilioni 3.825 sawa na asilimia 86) kilikwenda kwenye ushuru wa forodha uliotozwa kupitia vileo vilivyozalishwa na si kampuni.
Kiasi kingine cha fedha ambacho ni chini ya dola za Marekani bilioni 7 kinacholipa kodi kinaaminika ni “alama mwafaka ya mchango wa kodi katika shughuli za kawaida za uzalishaji,” ikijumlisha ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) inayolipwa na walaji na kodi ya mapato inayotokana na kodi ya wananchi.
Katika uchambuzi mwingine wa kiuchumi, SABmiller imesema kwamba sehemu kubwa ya kodi inayolipwa ni kutoka kwa wasambazaji na wateja katika utaratibu wa makato yao ya kiuchumi, ikijinasibu kuwa inawajibika kuilipa Serikali ya Afrika Kusini asilimia 1.7 kama kuwekeza sawa na Uganda, hivyo kushika nambari 4 kati ya walipa kodi wakubwa nchini Uganda.
Uchambuzi huo wa kiuchumi unaonekana kuwa ni halali na wa manufaa makubwa, lakini kubwa zaidi ni umuhimu wa kulipa kodi ya kampuni yenyewe, ambayo sehemu fulani hulipwa na walipa kodi wengine kwa niaba ya serikali.
Katika hatua nyingine, mapato yanaongezeka zaidi kwa watu wengine kulipa kodi wanapopata huduma maeneo mengine. Kiasi cha dola za Marekani milioni 620 kati ya dola bilioni 4.445 zinazolipwa na SABmiller ililipwa na kampuni yenyewe mwaka 2009-10.
Kampuni zinawajibika kutenda haki, kunufaika na huduma zinazotolewa na serikali kama raia wa kawaida. Zinahodhi mali na kufuata sheria za nchi na kutoa michango ya huduma za kijamii kama vile kujenga barabara, bandari, vitu ambavyo SABmiller haiwezi kusimamia badala yake inachangia tu.
Kampuni haziendi shule wala vyuoni badala yake zinasubiri kuombwa msaada zikatoe kwa jamii. Zimepewa ukomo wa kuwajibika ikiwa na maana kwamba hisa zao hazipotei wala hazifilisiki.
Manufaa yote haya yanatokana na kujipenyeza kuhudumia na kulipa kodi inayotumika kuboresha shughuli za kiuchumi kwa nchi zinazoendelea ambako SABmiller ina kampuni tanzu nyingi.
Je, unafahamu SABmiller na kodi yake inavyowajibika kwenye jamii? Usikose toleo lijalo la JAMHURI.