Uingereza, Ufaransa, na mataifa mengine yataongoza muungano huu, na watajaribu kuhusisha Marekani ili kupata msaada kwa Ukraine, alisema Starmer.

Huu ni baada ya mkutano wa kilele wa viongozi 18, wengi wao wakitoka Ulaya, wakiwemo Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, ambaye alieleza kuwa mkutano huo umeonyesha “umoja wa Ulaya katika kiwango cha juu sana, jambo ambalo halijawahi kuonekana kwa muda mrefu.”

Mpango huu unajiri baada ya mabishano makali kati ya Rais Zelensky na Rais wa Marekani, Donald Trump, katika Ikulu ya White House.

Katika mkutano na wanahabari, Starmer alieleza vipengele vinne muhimu vilivyokubaliwa na viongozi:

  1. Kuendelea kutoa msaada wa kijeshi kwa Ukraine na kuongeza vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Urusi.
  2. Amani yoyote ya kudumu lazima ihakikishe uhuru na usalama wa Ukraine, na Ukraine lazima iwe sehemu ya mazungumzo yoyote ya amani.
  3. Kuongeza uwezo wa ulinzi wa Ukraine ili kuzuia uvamizi wowote wa siku zijazo.
  4. Kuimarisha muungano wa walio tayari kutafuta suluhisho la amani kwa Ukraine na kuhakikisha amani ya baadaye ya nchi hiyo.Aidha, Sir Keir Starmer alitangaza nyongeza ya pauni bilioni 1.6 ($2 bilioni) kwa ajili ya kununua makombora 5,000 ya ulinzi wa anga, ikiwa ni sehemu ya msaada wa kijeshi zaidi kwa Ukraine. Nyongeza hii inakuja baada ya mkopo wa pauni bilioni 2.2 kutolewa ili kusaidia Ukraine kwa kutumia mali ya Urusi iliyozuiliwa.

Waziri Mkuu hakufafanua ni nchi gani zimekubali kujiunga na muungano huu, lakini Uingereza ilisema itaongeza msaada wake kwa vikosi vya ardhini na angani.

Ulaya lazima ichukue hatua nzito,” amesema Starmer, na kuongeza kwamba makubaliano haya yatahitaji msaada kutoka Marekani na lazima yakiwe na Urusi, lakini Moscow haitakiwi kulazimisha masharti yoyote.