Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Noel Barrot amelaani shambulizi dhidi ya Ubalozi wa Ufaransa mjini Kinshasa na waandamanaji Jumanne asubuhi.

“Mashambulizi haya hayakubaliki,” alisema katika chapisho kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), akiongeza kwamba waandamanaji “waliwasha moto ambao sasa umedhibitiwa”.

Moshi mwingi ulionekana ukifuka kutoka kwa ubalozi wa Ufaransa, baada ya sehemu yajengo lake lake kuchomwa moto.

“Juhudi zote zinafanywa ili kuwahakikisha usalama mawakala na raia wetu,” Barrot aliongeza.

Waandamanaji pia walilenga balozi za Rwanda, Kenya, Uganda, Ubelgiji, Uholanzi na Marekani.