Na Mwamvua Mwinyi, JamhuriMedia, Mafia 

Viongozi, Wadau wa Uvuvi, mazingira na Utalii kutoka Taasisi mbalimbali wakishiriki Kongamano la Uwekezaji kwenye Uchumi wa Buluu, lililofanyika katika ukumbi wa Halmashauri uliopo Chicco.

Mgeni rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Ndugu Rashid Mchatta amefungua kongamano hilo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani.

Akizungumza wakati wa Kongamano hilo, Mchatta amesema kwamba ni lengo la Serikali kuiona Mafia inapiga hatua katika masuala ya uchumi wa buluu kama ilivyo Zanzibar.

Bodi ya Utalii Tanzania ni miongoni mwa Taasisi zilizoshiriki ikiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Ramadhan Dau pamoja na Mkurugenzi wa bodi Bw. Ephraim Mafuru.