Mengi yamefanywa kuhusu umri wa Joe Biden na Donald Trump na jinsi wapiga kura wanavyowaangalia
Mtazamo huo ulikuwa zaidi kwa Biden mwenye umri wa miaka 81 ambaye kashfa, mashaka na makosa yake yyalikuwa gumzo – hasa katika wiki baaya mjadala wa rais.
Donald Trump, mwenye umri wa miaka 78, sasa atamiliki taji lisilotakikana la ‘mteule mzee zaidi katika historia ya urais’ na atarithi suala la umri kutoka kwa Biden ambaye amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuingia Ikulu ya White House.
Labda hicho ndicho hasa Chama cha Demokrasia kitataka kuangazia kwenye kampeni zake.