Na Mwandishi Wetu

SERIKALI ya Tanzania kwa kushirikiana na Ubaozi wa Nigeria imefanya kongamano kubwa la uwekezaji nchini humo lengo ikiwa ni kuvutia wawekezaji kutoka mataifa mbalimbali ndani ya Afrika.

Kongamano hilo ambalo lilifanyika kwenye miji ya Lagos na Enugu lililenga kuwaeleza wawekezaji wa Nigeria fursa mbaliambali za uwekezaji zinazopatikana hapa nchini.

Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekititi wa Bodi ya Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Dk. Binilith Mahenge.

Washiriki wa kongamano hilo nchini Nigeria

Akizungumza kwenye kongamano hilo, Dk. Mahenge, alielezea mageuzi makubwa ambayo Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan ameyafanya na kuvutia uwekezaji kutoka nje.

Alisema Tanzania imefanya mageuzi makubwa kwenye sheria na kanuni zinazosimamia uwekezaji na imeweka vivutio mbalimbali kwa wawekezaji wa ndani na wale wa kigeni.

“Katika kukuza diplomasia ya uchumi serikali ya Tanzania imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuboresha mazingira ya uwekezaji na biashara na hali hiyo imewavutia wawekezaji wengi kutoka mataifa mbalimbali,” alisema Dk. Mahenge.

Kwenye kongamano hilo ujumbe wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) ulifanya vikao na wenzao wa Chemba ya Biashara na Viwanda Lagos na walikutana pia na Chemba ya Biashara, Viwanda, Madini na Kilimo ya mji wa Enugu (ECCIMA).

Kongamano hilo lilijadili kuhusu sekta ya uzalishaji viwandani, ujenzi wa majengo, utalii, dawa, uchumi wa buluu, misitu, mifugo, huduma za kifedha, mafuta na gesi na uchakataji wa mazao ya chakula.

Mwenyekiti wa Bodi ya TIC, Dk. Binilith mahenge .
Washriki wakiwa kwenye picha ya pamoja
Please follow and like us:
Pin Share