Na Magrethy Katengu,JamuhuriMedia
Dar es Salaam
MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) imefanikiwa kuwa na ongezeko uandikishaji wa ada za bima kwa kampuni za umma na binafsi kwa. asilimia 7.4 kutoka tilion Tsh 1.15 ,mwaka 2022 hadi kufikia tilion 1.24 ,2023.
Akizungumza Novemba 2024 katika hafla ya uzinduzi wa taarifa hiyo ya utendajj wa soko la bima mwaka 2023 Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande amesema sekta ya bima ina jukumu la kuhakikisha inasaidia kujenga uchumi na kuwapa wananchi ulinzi imara wa afya na mali zao.
Ongezeko hili limechangiwa na hali halisi ya uwekezaji mzuri wa soko la bima chini ya Usimamizi wa Kamishna Dkta Baghayo Saqware na kwa kutoa elimu kupitia vyombo vya habari wananchi watambue umuhimu kwa kuwa na bima za afya na mali zao” amesema Chande
Naibu Waziri Chande amesema hivi karibuni Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ya ‘Bima ya Afya’ kwa wote ambayo kwa namna moja au nyingine inalenga kuona kila Mtanzania anakuwa na ‘Bima ya Afya’ hatua ambayo a inayopaswa kuchangamkiwa na kila mmoja wetu .
Hata huvyo , Chande amebainisha kuwa tafiti na tathmini mbalimbali zinaonesha kuwa soko la bima limekuwa likiongeza wigo wake wa kukua kila siku na kwamba kwa taswira ya uzinduzi wa mwaka huu inaonesha wazi kuwa soko hilo litaendelea kukua zaidi hivyo ni wakati muafaka sasa kwa TIRA kujipanga kikamilifu na kuhakikisha inaenda sambamba na ukuaji wa soko
TIRA pia imetakiwa kusimama mstari wa mbele na kuhamasisha uwekezaji, sambamba na kuhakikisha sekta ya bima inaendelea kuimarika maradufu.
Hiyo, kwa mujibu wa Naibu Waziri Chande amesema inapaswa kwenda sambamba na mamlaka hiyo kugeukia fursa za bima zilizopo kwenye sekta ya michezo nchini, sekta ambayo ameitaja kuwa inakua kwa kasi hivyo ni vyema ukafanyika utafiti ili kuona namna bora ya kuwafikia wadau wa michezo kwa ujumla wake
TIRA pia imetumia hafla hiyo kutoa tuzo kwa wadau na taasisi mbalimbali wanazofanyanao kazi kwa karibu au zinazofanya kazi zinazohusu bima na kutoa ushirikiano wa karibu kwao ikiwemo TRA, Jeshi la Polisi, Ofisi ya DPP, wanahabari, Mabalozi wa Bima.
Aidha hafla hiyo imehudhuriwa ikiwemo. viongozi na wadau mbalimbali kutoka taasisi za umma na sekta binafsi akiwemo Mwenyekiti wa Mabalozi wa Bima Tanzania ambaye pia ni Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Saidi, Waziri wa zamani wa Kilimo nchini ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vwawa (CCM) na Balozi wa Bima Tanzania Japhet Hasunga