Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Babati
Hatimaye tuzo ya Uhifadhi unaoshirikisha jamii ,iliyoshinda mwezi uliopita Taasisi ya Uhifadhi na Utalii ya Chem Chem Safaris, iliyopo eneo la hifadhi ya Jamii ya Wanyamapori ya Burunge(Buruge WMA), wilaya Babati Mkoa wa Manyara,imewasili nchini na serikali imepongeza.
Tuzo hiyo, imetolewa na Taasisi ya kimataifa African Travel and Tourism Association (ATTA) ya nchini Uingereza, ambayo ilishirikisha nchi mbali mbali duniani.
Tuzo hiyo,baada ya kufikishwa nchini sasa inatarajiwa kufikishwa serikalini na wizara ya Maliasili na Utalii kama.sehemu ya kuunga mkono jitihada kubwa za Rais Samia Suluhu kutangaza utalii na Uhifadhi nchini na kufungua milango katika.sekta ya Utalii na uhifadhi na sasa maelfu ya watalii wanakuja nchini.
Rais wa ATTA, Nigel Vere Nicoll, ndiye alitangazaushindi wa tuzo ikiwa ni sehemu ya vipengere vinane ambavyo vinatambulika na shirikisho la Utalii duniani vilivyokuwa vinashindaniwa.
“Baada ya majaji kupitia sifa za kila taasisi na pia kupokea maoni kutoka kwa watalii waliotembelea maeneo hayo, Taasisi ya Chemchem ndio ilikuwa mshindi wa kwanza wa jumla wa tuzo ,hasa baada ya kuweza kushirikisha jamii katika eneo la Burunge WMA katika uhifadhi na Utalii na jamii kunufaika “alisema.
Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Meneja Mkuu wa Chem Chem, Clever Zulu alishukuru ATTA kwa kuwapa tuzo hiyo na kutambua mchango wa Chem Chem katika Uhifadhi.
Zulu anasema tuzo hiyo sio ya Chem Chem peke yake bali ni tuzo ya Serikali, Tuzo ya Burunge WMA, Tuzo ya Wananchi wote hususani wa wilaya ya Babati mkoa Manyara ambao wamekubali ardhi yao itumike kwa uhifadhi na Utalii na wanashiriki kuitunza.
Afisa Wanyamapori mkoa Manyara, Felix Mwasenga alipongeza Chem Chem na Burunge WMA kwa ushindi wa tuzo hiyo,
Amesema serikali inatambua jitihada za uhifadhi ambazo zinafanywa na Chem Chem na sasa zinatambuliwa kimataifa.
“Tutaipokea taarifa za tuzo hii na itafikisha kwa viongozi wetu wa mkoa kuonesha jinsi mkoa Manyara unavyofanikiwa katika uhifadhi na Utalii.
“Tumeona ushindi huu na tunauthamini sana kwani utaongeza watalii kuja mkoa Manyara na hivyo kuongeza mapato ya serikali na wananchi”alisema
Taasisi nyingine zilizotangazwa kushinda, katika utoaji wa tuzo hizo uliofanyika London uingereza ni kutoka nchi za Uingereza, Namibia, Kenya na Botswana.
Kwa upande wake, Meneja wa hotel ya chemchem, Elizabeth Omboi na mkuu una maana kubwa kwao na utavutia watalii zaidi.
“Tumekuwa tukifanya shughuli za utalii wa hapa kwa kushirikisha jamii, tunatoa misaada kusaidia sekta za elimu, afya, mazingira na hata kusaidia makundi ya akina mama katika ujasiriamali”alisema Omboi.
Taasisi nyingine zilipata tuzo hizo ni Kisiwa cha chumbe kilichopo Zanzibar,Taasisi ya Asilia Afrika ya Uingereza, Lemala Camps and Lodges Tanzania.
Taasisi nyingine ni African Monarch Lodges ya Namibia,How Manyt Elephant ya Uingereza, Gamewatchers Safari&Porini Camp ya Kenya na Lets Go Travel Uniglobe ya Kenya.