Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Mbulu
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania ( KKKT) Askofu Dkt. Alex Malasusa amezindua jengo la Mama na mtoto la Hospitali ya Rufaa ya Kilutheri ya Haydom wilayani Mbulu Mkoani Manyara, lenye thamani ya sh.bil.6.5 kwenye jubilei ya miaka 70 ya Hospitali hiyo.
Akizungumza hizi karibuni kwenye Maadhimisho ya miaka 70 ya jubilee ya Hospitali hiyo Dkt. Malasusa amesema Hospitali hiyo Ina mchango mkubwa sana katika kulihudumia Taifa la Tanzania kwani jumla ya wilaya 7 na mikoa 4 wananchi wake wanapatiwa huduma katika hospitali hiyo tena Kwa kupatiwa huduma iliyo Bora kabisa.

Askofu Malasusa amesema Wamiaionanari walipofika Haydom walipelekq habari njema ya uwokovu na kuwasukuma kuanzishwa Hospitali hiyo iliyoanzishwa Mwaka 1955.
” Hospitali yetu hii ya haydomimeendelea na kuboresha miundombinu yake kwa kujenga jengo la Mama na mtoto kubwa na la kisasa lililogharimu jumla ya sh.Bil. 6.5, ni hilo mnaloliona hapo pembeni yetu Kwa mliochelewa wakati wa uzinduzi, nimelizundua hii Leo” amesema Askofu Dkt. Malasusa.
Aidha amesema Wamisionari walipopeleka wokovu Haydom wilayani Mbulu Mkoani Manyara ni kwa sababu ya wokovu ambalo ni jambo la Mbinguni tu, hivyo wametakiwa kutambua kuwa furaha ya kwenda Mbinguni lazima ianzie na hapa Duniani na si vinginevyo.

Mkurugenzi Mtendaji wa Tiba wa Hospitali ya Haydom wilayani Mbulu Mkoani Manyara Dkt. Paschal Mdoe Hospitali hiyo hutoa huduma kwa wananchi wa wilaya za Babati, Hanang’ na Mbulu za mkoani Manyara, wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Mkalama na Iramba mkoani Singida, Meatu mkoani Simiyu na Igunga mkoani Tabora na wilaya zingine mbalimbali.
” Tangu kuanzishwa kwa Hospitali hii Mwaka 1955 ilikua na vitanda 50 hadi Sasa tuna vitanda 420 yangu ilipopandishwa hadhi Mwaka 2010, ambapo hospitali ya rufaa ya Haydom inahudumia wagonjwa 105,296 wa nje na 14,020 wa ndani kwa mwaka” amesema Dkt. Mdoe.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara Michael Semindu ambaye ametimiza muda wa mwezi mmoja tangu ateuliwe na Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 70 ya hospitali ya rufaa ya kilutheri ya Haydom amesema Serikali itaendelea kuajiri wataalamu wapya wa afya na kuwapangia hapo ili kuendelea kutoa huduma Bora zaidi kwa jamii.

Mbali na hilo amewatanza wananchi wote wilayani humo kuhakikisha wanatambua kuwa Mwaka huu ni ,Waka wa uchaguzi Mkuu, na hivyo amewahakikishia kuwa utakua ni uchaguzi wenye amani.
” Mwaka huu ni Mwaka wa uchaguzi, tuombe kwenu Viongozi wa Kanisa na kuchaguliwa kwa pamoja tuombe, tuiombee nchi yetu na sisi kama Serikali tutahakikisha Mazingira yatakua salama, ulinzi na amani, Ombi langu kwenu nyote Kwa umoja wetu tuhakukishe tunadumisha amani , na mshikamano ” amesema Mkuu huyo wa Wilaya.



