Mhariri,

Hoja yangu ni kuhusu Jeshi la Mgambo. Kauli ni jeshi la akiba. Nimekuwa nikijiuliza maswali mengi bila majibu, kaulimbiu ni jeshi la akiba, lakini si kweli, bali ni jeshi la kutelekezwa na kukamuliwa. Haliendani na kaulimbiu.

Kila mwaka Serikali imekuwa ikiendesha mafunzo ya mgambo kwa kaulimbiu kuwa ni jeshi la akiba na kutumia fedha nyingi za walipa kodi ili kufanikisha jambo husika.

Lakini cha kushangaza baada ya mafunzo watu hawa hutelekezwa majumbani mwao na kuendelea kufanya uhalifu kwa kutumia uzoefu wa mafunzo na mbinu walizofundishwa. Hata kile kidogo walichopewa kama vile magwanda hupokonywa kwa kuambiwa uchangie jora na mashono.

Kama kweli ni jeshi la akiba linalothaminiwa kulingana na kaulimbiu, basi linapaswa heshima na kutendewa haki kama majeshi mengine. Mamlaka husika shughulikia kero hiyo.

Michael David,

Musoma – 0768-993 798