Na Magrethy Katengu, JamhuriMedia, Dar es Salaam
WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inalenga kuendelea kuchochea uandishi wa vitabu, usomaji na kukuza matumizi ya lugha ya kiswahili nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Aprili 7, 2025 amesema tuzo hizo zimejikita kwenye uandishi wa riwaya ,Tamthilia, hadithi za watoto,Ushairi, na tukio hilo linatarajiwa kufanyika Aprili 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam na mgeni ramsi atakuwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango.

“Tukio hili la tuzo ni kubwa na linatokea siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mwalimu Nyerere ambaye si tu alikuwa Rais wa Tanzania na mwanasiasa maarufu duniani na alikuwa mwandishi Mbunifu katika maishairi na kazi zake za kisaiasa, aliandika vitabu pia,” amesema Profesa Mkenda
Aidha Profesa Mkenda amesema lengo la tuzo hiyo ni kuhifadhi historia ya Nchi wapi tulipotoka na tulipo na tunapokwenda kisiasa kiuchumi,na kukuza uandishi bunifu na utamaduni wa watu kupenda kujisomea Vitabu mara kwa mara kwani vina hazina kubwa .
Washiriki hao walioteuliwa, 10 watawania tuzo ya uandishi wa vitabu vya riwaya, 10 vitabu vya tamthiliya, 10 vitabu vya ushairi na wengine 7 vitabu vya hadithi za watoto.

Naye Mwenyekiti wa Kamati wa tuzo hiyo, Profesa Penina Mlama amebinisha kuwa.Washiriki walioteuliwa, ni kama ifuatavyo ambapo Waandishi Wabunifu watawania tuzo ya uandishi wa vitabu vya riwaya, 10 vitabu vya tamthiliya, 10 vitabu vya ushairi na wengine 7 vitabu vya hadithi za watoto.
Hata hivyo amefafanua kuwa tuzo ya riwaya na waandishi wake kwenye wanaowania na watapatiwa zawadi ya simu janja ( Dk Abbas Amal), Taifa jipya (Ahmed Mwaita), Damu nzito (George Lauwo), Mashahidi kutoka kuzimu (Ibrahim Mkamba), Bweni la wavulana (Lucas Lubango), Kuokoka (Majaliwa Sued), Jeneza la taifa (Maundu Mwingizi), Udi na Uvumba (Philip Oyaro), Mlezi wa Vizazi (Richard Mziray) na Kilicho Chetu ( Zakaria Riwa).
Kwa upande wa ushairi, amesema wanaoshindanishwa ni Adili Mwinyiae (Yunge), Ally Mchanyato (Tuzo ya usomaji), Ally Isuka (Nikifa Msinizike), Bakari Makame (diwani ya tafakuri), Hussein Abdallah (Diwani ya Urathi wa Mjumu), Kombo Omar (Kisima cha Giningi), Mbaruku Mohammed (Utenzi wa Nana Mkombozi), Peter Komba (Mashairi ya Maisha), Said Ramadhan (Pendo la mama kiboko) na Sharifa Mussa (Pambazuko).“

Wanaowania tuzo hiyo kwa upande wa hadithi za watoto ni Corona Cermak (Tembo zimamoto), Hafidhi Makame (Siafu na Majimoto), Lilian Mbaga (Hatima yangu), Mwanacha Omary (Mwisho wa zarau), Paulina Lugabulila (Dieisha la Ajabu), Shifaa Feisal (Maua na Mji wa Maweni), Tune Salim (Maziwa ya Kuku).
“Kwa upande wa tamthiliya ni Ally Ngagesa (Kijarida), Bupe Kagute (Anne na Annelisa), David Shaba (Beti ya Mauti),Elithabeth Mahenge (Pambana), Faraji Manoni (Kovu la Maisha), Ignas Mkindi (Mwale wa Matumaini), Murungi Katabarula (Zaidi ya Majirani), Said Kileo (Mwangaza ) Sajida Athumani (Mwangaza wa Mvita) ma Tyatawelu Kingu (Alama ya Kuzaliwa),” Amesema Profesa Mlama
Aidha amesema mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Sh. Milioni 10, na cheti na muswada wake kutachapishwa na serikali na kisha kusambazwa shuleni na maktaba za taifa huku mshindi wa pili atapata Milioni 7 na cheti na mshindi wa tatu ataondoka na milioni 5 na cheti.
Naye Mkurugenzi Mkuu TET, Aneth Komba amesema kupitia tuzo hiyo yenye lengo la kukuza sekta ya uchapishaji wameweza kuchangia kuikuza sekta hiyo kwani kila mwaka wanakuwa na mzabuni mmoja wa uchapishaji ambaye ndio uchapisha vitabu kwa mwaka wa fedha.
Hivyo wamefanya kitu cha tofauti kwani mshindi vitabu vyake kuchapishwa na serikali na kusambazwa katika shule zote za serikali nchini kwa uwiano wa shule moja vitabu 14.

