Na Mary Margwe, JamhuriMedia, Mbulu

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Abubakar Kuul na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Joseph Mandoo na Mbunge wa Jimbo hilo Flatei Massay kwa kuwa na miradi yenye Viwango, ambapo amesema wanaondoka Mbulu DC wakiwa wameridhika na kwamba kufanya hivyo ni kumtendea haki DKT. Samia na hata wao pia.

Hayo ameyasema Leo Julai 14,2024 wakati alipokua akizungumza kwenye makabidhiano ya Mwenge wa uhuru katika Kijiji cha Guneneda Kata ya Tlawi mbele ya mkuu wa Wilaya hiyo Veronica Kessy.

Kiongozi Mnzava amesema eye pamoja na WAKIMBIZA MWENGE wa uhuru Kitaifa wametembelea, wamekagua miradi 7 Kwa kufanya kazi ya ufunguzi, kuweka mawe ya msingi, kutembelea miradi mbalimbali ambayo Ina Viwango vya kumuheshimisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan.

” Tunaondoka Mbulu DC tukiwa tumeridhika kabisa ya kwamba MMEMTENDEA HAKI Dkt.Samia na hata sisi pia , ila msituache na sisi kwenye dua”amesema kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru Kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava.

” Tunaomba hii miradi iendelee kusimamiwa kikamilifu ili iweze kukamilika Kwa ile ambayo Iko katika hatua mbalimbali, lakini kubwa ilindwe na kuitunza” amefafanua Mnzava.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Abubakar Kuul amesema Mwenge wa uhuru ulipokua katika Halmashauri hiyo ulifikia miradi 7 yenye thamani ya sh.bil.46,355, 332,496.44.

Kuul amesema kati ya miradi hiyo mmoja ulikua ni WA ufunguzi, miradi miwili ya kuwekewa jiwe la msingi, mitatu ya kutembelewa na kuonwa na mmoja wa kukabidhi vifaa vya kufundishia, kujifunzia na Michezo Kwa wanafunzi wenye mahitaji Maalum.

Aidha Kuul amefafanua kuwa Mwenge ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu umeelimisha na kuueneza ujumbe Mkuu wa Mwenge wa uhuru 2024 usemao” Uhifadhi wa Mazingira na uchaguzi wa Serikali za Mitaa chini ya kauli mbiu isemayo ” Tunza Mazingira na Shiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu”