Mhariri,
Mimi ninaitwa Issa Juma Dang’ada, ninaishi mjini Nzega, mkoani Tabora. Ni Mjumbe wa Baraza la Katiba Wilaya ya Nzega.
Kero yangu ni kwamba, TUME YA KATIBA ilitangaza kuwa mchakato wa kuanza mabaraza ya Katiba utaanza 12,7/2013, hivyo wajumbe wote 20,000 nchi nzima tukapewa Rasimu ya Katiba tuisome mwezi mzima bila posho!
Wakati TUME imepewa fedha nyingi mpaka za ukimwi! Cha ajabu mpaka leo hatujalipwa posho tangu 12/7/2013yo! Je, Jaji Warioba anaweza kufanya kazi kwa staili hiyo?
Barua ya mwaliko inaonesha kuwa wajumbe tutalipwa siku nne wakati TUME YA KATIBA imetangaza siku 54 za mabaraza ya Katiba. Je, TUME imepeleka wapi malipo ya siku 50 zinazobaki?
TUME inataka kuiba posho za wajumbe 20,000 nchi nzima! Uadilifu uko wapi kwenye tume hiyo? Nimeamua kutoa kero hii kwa faida ya Watanzania.
Issa Juma Dang’ada, Nzega