Tukiwa tunaelekea kupokea bajeti mpya ya serikali ya 2024/2025 ikijadiliwa bungeni kwa mujibu wa sheria, pia nasi katika jamii tukieendelea kuifuatili kwa ukaribu na umakini mkubwa.

Hii haimaanishi kwamba suala hili ni la wanasiasa sio kwakuwa bajeti ndio taswira na mwelekeo wa uchumi wanchi kwa kipindi cha mwaka.

Tumeshudia katika bajeti hii kwa kiasi kikubwa inategemea mapato ya ndani kwa asilimi 70 na hii inathibitisha ile falsafa ya kujitegemea.

Taifa limefika hatua nzuri kama ilivyo bainishwa katika misingi ya azimio la Arusha 1967 moja kati ya misingi yake ni kujitegemea, kwa msingi huo wa kuanza kujitegemea kama taifa hili ni jambo la kujivunia kwa kuwa tumepiga hatua nzuri.

Matunda haya ni utekelezaji wa ilani na sera za Chama Cha Mapinduzi tukizingatia falsafa isemayo uhuru wa kweli ni kuwa huru kiuchumi.

WAJIBU WA MWANANCHI
Kwakuwa serikali imethibitisha kuwa dhana yakujitegemea au kutegemea mapato ya ndani ya kikodi na ushuru pamoja na mikopo ya ndani ya nchi hivyo sisi wananchi hatuna budi kuunga mkono serikali kwa kulipa kodi ya mapato na ushuru bila shuruti ili kutegemeza Serikali kutekeleza miradi ya kiuchumi,kimkakati na kijamii.

Kwanza jamii ifahamu kuwa kila mtanzania ana shiriki katika kulipa kodi yaani direct tax na indirect tax. Pia Watumishi wa umma wote ni walipa kodi kwa maana kwamba kupitia mishahara yao wana katwa kodi kwa mujibu wa sharia.

Nimesema hivi ili kuondoa dhana kwamba walipa kodi ni wafananya biashara hio dhani ni potofu hivyo kila mtanzania anashiriki katoika kulipa kodi mfano unapo nunua soda unakua umelipa kodi ,kiberiti ete.

Hivyo hii dhana kuwa wafanyabishaashara wana msururu wa kodi ni dhana ambayo inatakiwa ipuuzwee ama ieendelee kutolewa elimu na ufafanuzi kwa wananchi ili iweze kueleweka.

Kwa Taifa letu TRA wana fanya kazi nzuri na kubwa ya kukusanya mapato ya serikali wakisisitiza kutoa elimu kwa mlipa kodi marakwamara kupitia vyombo vya habari na matangazo yaliyo wekwa katika maeeneo mbalimbali ikiwemo masokoni.

Pia katika matangazo hayo yana sisitiza kuomba stakabadhi ya malipo baada ya kununua bidhaa hivyo kila mmoja wetu ana wajibu wakufanya katika kusaidia swala la ukusanyaji kodi kwa kuhakikisha tunaomba stakabadhi ya malipo pindi tununuapo bidhaa.

Kwa ufupi wote tuna wajibu wa pamoja yaani collective responsibility ya kuunga mkono serikali katika dhima nzima ukusanyaji kodi.


BANGO LA TRA SOKO KUU ARUSHA

Jambo la kwanza ni matumizi mazuri ya EFDS hii itarahisha kazi kwa mmlaka kufanaya makadirio ya kodi kwa usahihi bila manung’uniko.

Pili; kutumia wataalam (accountants) katika kufunga mahesabu ya mauzo hii itasaidia mamlaka kufanya makadirio ya kodi kwa usahihi na pia biashara kustawii.


Tatu; Hulka ya uzalendo na upendo kwa Taifa .kimsingi kodi ndio msingi mkubwa wa maeendeleo ya taifa letu hivyo kila mmoja wetu aone haja ya kulipa kodi kwakuwa maeendeleo ya nchi yana hitaji kodi na walipa kodi ni sisi wanannchi.”Tulipe kodi kwa maeendeleo ya taifa letu”

Mfano hivi karibuni tumeshuhudia mgomo wa wafanya biashara wakifunga biashara kwa kigezo cha kuhitaji punguzo la baadhi ya kodi hususan VAT na ushuru wa huduma(service levy) hii changamoto bilashaka ni uzalendo hafififu miongoni mwetu hivyo somo la uzalendo lieendelee kufundishwaa ili kuepusha hizi changamoto.

WAJIBU WA SERIKALI NA MAMLAKA ZA UKUSANYAJI KODI
Moja kati ya kazi kubwa ya serikali ni kukusanya kodi kutoka katika vyanzo vyake. Na hili limekuwa likiwezekana kwa serikali kueendelea kuweka mazingira rafiki kwa walipa kodi kwa upande wa watumishi wa umma wamepandishiwa mishara na stahiki zao hivyo hata makato ya kaodi yamekuwa himilivu.

Pia kwa upande wafanyabishara Serikali imeendelea jenga masoko ya kisasa mfano maboresho ya soko la kimataifa la kariakoo dsm hii yote ni kuweka mazingira rafiki ya biashara.

Pia mifumo ya kidigiti yaani TAUS,mfumo unao wmezesha mlipa kodi kujipatia namba ya malipo mwenyewe (control number) hii imesaidia kupunguza msongamano usio wa lazma katika ofisi za srikali ili kupata huduma.

Mbali na hayo serikali inazingatia na kuhakikisha mambo yafuuatayo;

Ulinzi na usalama wa nchi. Kwa hili tumeshudia taifa letu likiwa na usalama wa kutosha hali inayo shajihisha biashara na shughuri za usafirishaji. Mfano Soko kuu la majengo Dodoma na soko la machinga Dodoma yakifanya kazi masaa 24.

Pia usafirishaji nao ni masaa 24. Hii imepelekea mzunguko wa fedha kuwa mkubwa na hatimaye wigo wa mapato ya serikali kuongezeka.kwa hili swala la usalama hatuna budi Kuvipongeza vyombo vya ulinzi na usalama kwa kazi nzuri ya kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama kiukweli.

Pia vibali vya uwekezaji na kanda huru za kiuchumi (EPZD) na maboresho makubwa ya malango ya mapato ikiwemo bandari na ukuzaji wa sekta mtambuka za kiuchumi hususani utalii,kilimo madini na uvuvi.kwa hili serikali imepiga hatua kubwa kwa kupunguza urasimu wa usajili wa makampuni na utoaji leseni kupitia mfumo wa kieletroniki kupitia BRELA.

Hii nayo imedhihirisha kuwa Serikali iko mathubuti katika kushajihisha mapato.

Elimu ya kodi hili jambo Serikali inafanya kazi kupitia vyombo vya habari tumeshudia mara kadhaa TRA ikitoa elimu juu ya ulipaji kodi.Pia katika somo la urai tuna jifunza kuwa wajibu wa mwanachi mi kulipa kodi kwa maeendeleo ya Taifa.

Kuna huu msemo una sema “ mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe” Sisi wa Tanzania tumeone mafanikio makubwa ambayo nimatokeo ya ulipaji kodi kwa Taifa letu. Kujitegemea kama taifa tumeanza kuona taifa limeanza kujitegemea katika bajet kwa mapato yake ya ndani kwa asilimia 70 hii ni bila udhamini wa wadau na washirika wa maeendeleo japo bado tuna wahitaji ila mwelekeo mi mzuri wa kujitegemea. Hili ni jambo la kupongezwa na kila m Tanania hasa wale wenye fikra za kizalendo.

Huduma za kijamii.hapa taifa limeendelea kutoanhuduma za jamii kwa kutumia mapato ya ndani.mfano kutoa elimu bila malipo kuanzia ngazi ya awali mpaka kidato cha sita,pia kulipia elimu juu ,huduma bure za afya huduma ya mama wajawazito na motto,wazee na makundi maalum.huu niuthibitisho tosha kuwa kodi inayo lipwaa intija kwa taifa letu hivyo wananchi tulipe kodi kwa maeendeleo ya nchi yetu.

Miradi ya kimkakati. Tumeshuhudia miradi ya mingi ya mingii ya kimkakati ikiwemo miradi ya maji na miundombinu ikiwemo daraja la mto wami,ujenzi wa masoko ya kisasa mfano soko la job ndugai Dodoma,soko kuu la njombe ni kwa uchache.haya yote ni matokeo ya kodi ya ndani hivyo wananchi hatuna budi ya kuunga mkono serikali kwa kulipa kodi tulipeni kodi kwa maeendeleo ya Taifa letu.

Nahitimisha kwa kusema kuwa haya mafanikio ni kutokana baraka ambazo Mungu amikirimia nchi yetu kupata viongozi wa zalendo,mahiri na mathubuti tangu tupate uhuru 1961.

Hivyo kwa awamu hii ya sita inayoongozwa na Dk Samia Suluhu Hassani Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa amekuwa nembo na taswira nzuri ya kushajihisha ulipaji wa kodi kwa kuongeza wigo wa mzunguko wa fedha.

Mfano kupitia filamu ya Royal Tour ambayo imeleta ongezeko la watalii wengi na miongoni mwao wawekezaji hivyo Tuna mpongeza Rais wetu. Pia Diplomasia ya uchumi na mikutano ya kimataifa hii inavitia wawekezaji ,tekinolojia na hata fedha za kigeni kwa wageni wengi kuja nnchini ina pelekea kuwa na mzunguko mkubwa wa fedha hatimaye kodi inaongezeka.

Hivyo Watanzania hatuna budi ya kueendeea kuwa wazalendo wa kweli kwa kulipa kodi na sio kuwa na mlengo hasi juu ya kodi. Mfano ushuru wa huduma ni msingi mkubwa wa makusanyo katika halimashauri zetu hivyo mawazo ya kutaka ifutwe ni kuziaangamiza Halimashauri zetu jambo ambalo halipaswi hata kufikiriwa cha msingi ni kuendelea kuelimishana kadri iwezekanavyo kuhusu Mantiki, tija na ulazima wa kulipa kodi.

Imeandaliwa na John Francis Haule, mkuu wa soko kuu la Arusha. Anapatikana kwa simu 0765717987 au 0711993907 Barua [email protected]