Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Kamishna Msaidizi wa Polisi Benjamin Kuzaga amewataka Maafisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kulinda na kuitunza miti iliyopandwa katika maeneo yao.

Kauli hiyo ameitoa leo Februari 14, 2024 wakati akiongoza zoezi la upandaji miti kwa Polisi Mkoa wa Mbeya katika uwanja wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Mbeya.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa, zoezi la upandaji miti katika maeneo ya kambi za Polisi, vituo vya Polisi na maeneo mengine ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus Wambura.

Aidha, ameongeza kuwa zoezi hilo litafanyika katika Wilaya zote sita za Kipolisi Mkoa wa Mbeya ambapo kila askari amekabidhiwa mche wa mti kwa ajili ya kupanda na kuhakikisha anautunza ili kufikia malengo ya Jeshi na nchi kwa ujumla.

Kamanda Kuzaga amesema kuwa, zoezi lililofanyika leo, jumla ya miche ya miti ya matunda na kivuli elfu moja aina ya Kassuarina, Pinuspatula, Misongwa na Mizambarao imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya.

SHARE