Rais wa Marekani Donald Trump amemtupia lawama rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kwa kukataa kukubali kulipoteza eneo la Crimea ambalo tayari linakaliwa kimabavu na Urusi ili kumaliza vita baina ya nchi hizo mbili.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari Trump amesema makubaliano ya kumalizika kwa vita yalikuwa “karibu mnoo” na Urusi iliukubali mpango huo wa Marekani lakini Rais Zelensky wa Ukraine aliyakataa masharti hayo ambayo Marekani inasema yangeliweza kuumaliza kabisa mzozo huo.
Katika hatua nyingine, Zelensky amejibu kauli hiyo kwa kuchapisha kwenye mtandao wa kijamii chapisho kuhusu Crimea la 2018 la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani wa wakati huo Mike Pompeo ambalo lilisema Washington “inakataa jaribio la Urusi kuitwaa Crimea.”
Hapo jana maafisa wakuu wa Ukraine walikuwa mjini London kwa mazungumzo juu ya mzozo huo na wawakilishi kutoka Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Marekani.