Trump na Putin wazungumza kwenye simu kuhusu vita nchini Ukraine
Rais wa Mteule wa Marekani amemtaka mwenzake wa Urusi kutoendelea kuchochea vita nchini Ukraine, kulingana na Gazeti la “Washington Post”.Donald Trump alizungumza na Rais wa Urusi Vladimir Putin siku ya Alhamisi na kumtaka asichochee hali ya kuongezeka kwa vita nchini Ukraine, Gazeti la kila siku la Marekani la Washington Post liliripoti siku ya Jumapili, Novemba 10.
Haya yatakuwa mazungumzo ya kwanza ya simu kati ya wawili hao tangu Donald Trump ashinde uchaguzi wa urais wa Marekani siku ya Jumanne ya wiki iliyopita dhidi ya Kamala Harris wa chama cha Democrat.
Walijadili lengo la amani katika bara la Ulaya na Donald Trump alisema anatumai kuwa na mazungumzo ya kufuatilia ili kujadili “kusuluhisha vita vya Ukraine hivi karibuni”, kulingana na vyanzo ambavyo havikujulikana vya Gazeti la kila siku la Marekani.
Wakihojiwa na shirika la habari la AFP, wasaidizi wa Donald Trump hawakuthibitisha habari hii.
Biden na Trump kufanya mazungumzo katika Ikulu ya White House Jumatano
Masuala ya sera za kigeni yatakuwa kwenye menyu ya mkutano kati ya Joe Biden na Donald Trump uliopangwa kufanyika White House siku ya Jumatano katika kujadili jinsi ya kukabidhaiana madaraka.
Donald Trump, ambaye atarejea Ikulu ya White House mnamo Januari 20, amekuwa akidai mara kwa mara kuwa anaweza kumaliza vita “kwa siku moja”, bila hata kuelezea jinsi atafikia kumaliza vita hivyo. Lakini hii pengine inaweza kuhusisha mpango ambao utahitaji kyiv kukabidhi sehemu ya eneo lake kwa Moscow.
Kremlin ilibaini siku ya Jumapili kwamba rais mteule wa Marekani alikuwa ametuma “ishara chanya” wakati wa kampeni kuhusu mzozo huo, kwani alizungumza juu ya uwezekano wa “amani” na hakuonyesha “nia ya kuisababishia Urusi ushindi wa kimkakati.”
Ili “kuiweka Ukraine katika nafasi imara zaidi kwenye uwanja wa vita ili iwe katika nafasi yenye nguvu zaidi katika meza ya mazungumzo,” utawala wa Biden unapanga kutumia dola bilioni sita zilizosalia kabla ya kuwasili kwa Donald Trump madarakani.
Donald Trump pia tayari alizungumza na Volodymyr Zelensky siku ya Jumatano. Mazungumzo ambayo bilionea Elon Musk alishiriki na kuelezewa kama “bora” na rais wa Ukraine.