Rais wa Marekani Donald Trump amepanga kuwaondoa kazini zaidi ya watu 1,000 walioteuliwa na utawala wa Rais wa zamani Joe Biden.
Miongoni mwa watu watakaoondolewa kazini ni mpishi mashuhuri Jose Andres na jenerali mkuu wa zamani Mark Milley.
“Ofisi yangu ya utumishi wa Rais iko katika mchakato wa kuwatambua na kuwaondoa zaidi ya wateule elfu moja wa Rais kutoka kwa utawala uliopita, ambao hawaambatani na maono yetu,” alisema.
Hatua hiyo imezua wasiwasi kwamba rais anapanga kuwaondoa wote walioteuliwa wakati wa utawala wa Biden na kuwaweka watu anaoamini watakubaliana na ajenda zake.