Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kwamba Washington, inapiga hatua katika mazungumzo yake ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine.

Rais wa Marekani Donald Trump amesema anaamini kwamba Washington, inapiga hatua katika mazungumzo yake ya kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine, lakini amekataa kutoa maelezo kuhusu mawasiliano yoyote aliyoyafanya na Rais wa Urusi Vladimir Putin.

Akizungumza na waandishi wa habari ndani ya ndege ya Air Force One wakati akielekea katika mchezo wa Super Bowl, Trump alidokeza kuwa yeye na Putin walikuwa wakiwasiliana. Trump kufanya mkutano na Putin Februari au Machi.

Alipoulizwa kama amefanya mazungumzo na Putin tangu awe rais Januari 20 au kabla, Trump alikiri kuwa amekuwa na mawasiliano na anatarajia kufanya mazungumzo zaidi.

Aidha, Rais Trump ameongeza kuwa Marekani inawasiliana na pande zote mbili za Urusi na Ukraine. Trump aliahidi kumaliza vita lakini bado haijawekwa wazi jinsi atakavyofanikisha hilo.