Mahakama ya Juu nchini Marekani imeamua kuwa Colorado haiwezi kumuengua Donald Trump kwenye mchujo wake wa urais wa chama cha Republican.
Jimbo la Colorado lilimzuia Trump kushiriki kura ya jimbo hilo mnamo Desemba, ikinukuu kifungu cha uasi katika Katiba na akihoji kuwa rais huyo wa zamani ndiye aliyechochea ghasia za 2021 Capitol huko Washington, D.C,
Uamuzi wa mahakama unasafisha njia kwa Trump kushindana katika mchujo. Uamuzi huo ulikubaliwa na majaji tisa wa Mahakama ya Juu.
Trump ndiye mshindani wa mbele wa uteuzi wa chama cha Republican na anaonekana huenda akakabiliana na Rais wa chama cha Democratic, Joe Biden katika uchaguzi mkuu wa Novemba.
Colorado, pamoja na majimbo mengine 14, watapiga kura Jumanne katika mashindano ya marathon yaliyopewa jina la Super Tuesday.
Rais huyo wa zamani anatarajiwa kumshinda mpinzani wake pekee aliyesalia, Balozi wa zamani wa Umoja wa Mataifa Nikki Haley.