Wakati Donald Trump amepata ushindi unaomrejesha Ikulu ya White House, bado si rais rasmi – na itachukua zaidi ya miezi miwili kabla ya kurejea katika Ofisi ya Oval.
Makabidhiano ya madaraka ya Marekani ni tofauti sana na jinsi mambo yanavyofanyika nchini Uingereza. Mnamo Julai, Sir Keir Starmer aliapishwa kama waziri mkuu ndani ya saa chache baada ya uchaguzi kumalizika na kabla ya Rishi Sunak hata kubeba vitu vyake.
Trump ataapishwa Januari 20 na Joe Biden atasalia madarakani hadi wakati huo – ingawa atakuwa na kikomo cha kisiasa katika kile anachoweza kufanya.