Donald Trump amemteua Seneta wa Ohio JD Vance kuwa makamu wake wa rais.

Wajumbe wa Kongamano la Kitaifa la chama cha Republican walimchagua rasmi Bw Vance, 39, Jumatatu baada ya Trump kutangaza kwenye mtandao wake wa kijamii kuwa amemchagua baada ya “kutafakari na kufikiria kwa muda mrefu”.

Bw Vance ni mjasiriamali aliyeelimishwa na mwandishi wa riwaya ya kumbukumbu ya maisha yake ya Hillbilly Elegy iliyokuwa na mauzo mazuri ambayo iligeuzwa kuwa filamu.

Hapo awali alimkosoa mgombea mwenza wake mpya, akipendekeza kwa faragha kwamba Trump anaweza kuwa “Hitler wa Marekani”, lakini amekuwa mfuasi mkubwa.

Mnamo mwaka wa 2016, wakati Donald Trump alipomchagua Gavana wa Indiana Mike Pence kama mgombea mwenza wake, ilitazamwa na wengi kama juhudi ya kupata kura za Wakristo Wainjilisti ambao wanaweza kuwa na wasiwasi wa kumuunga mkono Trump.

Wakati huu, amemchagua JD Vance. Na kama chaguo lake la awali, uteuzi wa seneta huyo unatoa mwanga kuhusu mkakati wa kampeni ya rais huyo wa zamani – na, pengine, jinsi angetawala ikiwa atarejea Ikulu ya Marekani.

Chaguo linapendekeza Trump anajua uchaguzi huu atashinda na kushindwa katika majimbo machache yanayokuwa na ushindani mkubwa ya Midwest.

Kwa historia yake, Vance anaweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuungana na kuwatia nguvu wapiga kura wazungu, wanaofanyakazi ambao walimpa ushindi Trump mnamo 2016.

Rais huyo wa zamani alisema hayo, katika ujumbe wake mtandaoni akitangaza uamuzi wake, na kusema kuwa mgombea mwenza wake “atazingatia sana watu aliowapigania mno, wafanyikazi wa Marekani na wakulima huko Pennsylvania, Michigan, Wisconsin, Ohio, Minnesota na zaidi”.

Trump aliendelea kusifu huduma ya kijeshi ya mteule wake.

Na ikiwa rais huyo wa zamani atarejea ikulu mwaka ujao, Vance atajiunga mara moja kwenye mazungumzo ya uteuzi wa urais wa chama 2028.

Please follow and like us:
Pin Share