Rais Donald Trump amehudhuria mkutano wa chama cha Republican akikaribishwa kwa shangwe na nderemo.

Hii ni mara ya kwanza kwake kuonekana kwenye hafla kubwa ya umma tangu jaribio la mauaji dhidi yake kwenye mkutano wa kisiasa siku ya Jumamosi.

Bandeji iliyokuwa kwenye sikio la Trump ilionekana wazi huku akichukua nafasi yake karibu na mgombea mwenza wake, JD Vance.

Wafuasi wa Republican walikuwa na furaha isiyokifani.

Walianza kuimba “U-S-A, U-S-A” na kuendelea kusema “Pambana! Pambana! Pambana!” huku wakirusha ngumi hewani, ishara kwamba wengi hapa wamemkubali baada ya Trump kuonyesha kuwa imara alipokuwa anashuka jukwaani baada ya kupigwa risasi huko Pennsylvania.

Wengine waliokuwepo ni pamoja na wanafamilia, kama vile wanawe Eric na Donald Jr.

Rais huyo wa zamani alionekana kutabasamu na kupiga makofi wakati wote wa hotuba.

Mara kwa mara aliwageukiwa Vance na Donald kutoa maoni juu ya kile kilichosikika.

Please follow and like us:
Pin Share