Donald Trump amejisalimisha huko Georgia kwa tuhuma za kupanga njama ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa jimbo hilo wa 2020 katika hatua ya kukamatwa kwa mara ya kwanza kwa rais wa zamani wa Marekani.
Trump alilazimika kulipa bondi ya dhamana ya $200,000 (£160,000) ili aachiliwe kutoka jela ya Atlanta wakati akisubiri kesi yake.
Baadaye, alielezea kesi hiyo kama “ukiukaji wa haki”.
Ilikuwa ni mara yake ya nne kukamatwa katika kipindi cha miezi mitano katika kesi ya jinai, lakini hii ilikuwa picha yake ya kwanza ya kupigwa na polisi.
Trump baadaye aliweka ujumbe kwenye X, ambayo zamani ilijulikana kama Twitter, kwa mara ya kwanza tangu Januari 2021.
Alishiriki anwani ya tovuti yake na picha hiyo yenye herufi kubwa na nukuu: “Uingiliaji wa uchaguzi. Usijisalimishe kamwe!”
Anajiunga na orodha ya watu mashuhuri wa Marekani ambao wamewahi kukamatwa, ikiwa ni pamoja na Elvis, Frank Sinatra, Al Capone na Dk Martin Luther King Jr.